Katika zama za utawala wa Uthmaniyyah (Ottoman Empire), tawala zote
ambazo zilikuwapo katika bara la Uarabu, kila jimbo lilikuwa na maofisa
waliokuwa wameteuliwa kutoka serikali kuu. Baadaye, kila mkoa isipokuwa Hijaz
ilikuwa mikononi mwa wale walioweza kuzinyakua na kuwa tawala za Kifalme.
Imani za Mawahhabi zilizoenezwa na Muhammad ibn ‘Abd al - Wahhab
zilikuwa zimeshabadilika kuwa katika sura za kisiasa katika kipindi kifupi
katika mwaka 1150 A.H.( 1737) na zilienea Bara zima la Arabia. Baadaye, kwa
amri za Khalifa wa Istanbul, Muhammad ‘Ali Pasha, Gavana wa Misri, aliikomboa
Arabia kwa msaada wa majeshi ya Misri.
‘Abd al-‘Aziz ibn Muhammad, aliyewaamini Mawahhabi, alitangaza vita
kwa mara ya kwanza katika 1205 A.H. (1791) dhidi ya amir wa Makkah, Sharif
Ghalib Effendi. Wao walikuwa wamekwisha eneza Uwahhabi kisirisiri hadi hapo.
Wao waliwaua na kuwatesa Waislamu wengi mno, kuwachukua wanawake na watoto wao
mateka na kuzipora mali zao zote.
Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab alitokana na kabila la Bani Tamim.
Alizaliwa katika kijiji cha Uyaina karibu na mji wa Huraimila huko katika
jangwa la Najd, mwaka 1111 A.H.(1699) na kufa 1206 A.H.( 1792). Hapo awali
alikuwa na nia ya kufanya biashara, hivyo alisafiri hadi Basra, Baghdad, Iran,
India na Damascus, ambako kote huko alijipatia sifa la jina kama Sheikh wa Najdi kwa sababu za ujanja na
tabia yake.Yeye aliona na kujifunza mambo mengi katika sehemu hizi na hivyo
akawa na hamu ya kuwa kiongozi mkubwa. Hivyo ili kutaka kutimiza hamu yake hiyo
ilimbidi abuni njia moja iliyokuwa tofauti na njia zinginezo ili aweza kutimiza
malengo yake, na kwa kujitayarisha kwa hayo, alianza kuhudhuria mihadhara ya
maulamaa wa Kihanbali waliokuwapo katika Mji Mtukufu wa Madinah na baadaye huko
Damascus kwa kipindi fulani. Wakati aliporejea Najd, alianza kuandika makala
juu ya maudhui ya dini kwa ajili ya wanakijiji wake.Katika kuandika makala
hayo,yeye alikuwa akiongezea fikara zake alizokuwa amezipata kutoka makundi ya bid’a ya Mu’tazila na wengineo.
Wanakijiji wengi waliokuwa masikini majahili, hususan wakazi wa Dar’iyya na
chifu wao jahili, Muhammad ibn Sa’ud, walikuwa wakimfuata Muhammad ibn 'Abd
al-Wahhab. Waarabu walikuwa wakiheshimu mno ukabila na kwa kuwa Muhammad ibn
'Abd al-Wahhab alikuwa si kutoka kabila maarufu, basi alimtumia Muhammad ibn
Sa’ud kama chombo kwa kutangaza fitna
yake mpya aliyokuwa ameiita Uwahhabi.
Yeye alijitambulisha kama Qadhi (mkuu
wa mambo ya dini ) na Muhammad ibn Sa’ud kama Hakim (mtawala). Kwa hila zake alikwishafanya mabadiliko katika katiba yao kuwa wao hawatarithiwa na mtu
yeyote yule isipokuwa watoto wao tu.
No comments:
Post a Comment