COCA COLA NA PEPSI COLA NI HATARI KWA AFYA YAKO
Utafiti uliofanywa na shirika la National Consumer Institute (INC) la Ufaransa unaonesha kuwa vinywaji baridi viitwavyo coca cola na pepsi cola ni miongoni mwa vinywaji baridi vyenye pombe ndani yake. Kiwango cha alcohol kinafikia 10mg kwa lita ambayo ni sawa na 0.001% alcohol.
Kama haitoshi, vinywaji hivyo vina chembe chembe za sumu kama Tarpenes na E150d (sulphate ammonia caramel), kemikali ambayo imetangazwa na serikali ya jimbo la California huko Marekani kuwa ni kemikali hatari kwa afya. Baada ya tangazo hili Makampuni hayo yameahidi kutokuweka chembechembe hizo katika vinywaji wavyouza Marekani lakini katika nchi nyingine bado wanaweka kemikali hizo.
No comments:
Post a Comment