Saturday 7 July 2012

Spika wa Bunge la Syria: Uturuki, Saudi Arabia na Qatar zinaunga mkono magaidi












Spika wa Bunge la Syria ametangaza kuwa, nchi za Saudi Arabia, Uturuki na Qatar zinayasaidia makundi ya kigaidi yanayotekeleza mauaji katika ardhi ya Syria.
Spika Muhammad Jihad al-Laham amezikosoa vikali Saudia, Uturuki na Qatar kwa kuchochea machafuko ndani ya ardhi ya Syria ikiwa ni pamoja na kuyaunga mkono makundi ya kigaidi katika nchi hiyo.

Amesema, nchi hizo zimekuwa zikitoa misaada ya kifedha na kilojistiki kwa makundi ya kigaidi nchini Syria ili kukabiliana na wananchi pamoja na serikali ya Damascus. Spika wa Bunge la Syria ameituhumu Uturuki kwamba, inafuata siasa za Marekani katika kadhia ya nchi hiyo; kwani silaha nyingi zinazoingia Syria kwa ajili ya makundi ya kigaidi zinapitia katika mpaka wa nchi hiyo na Uturuki.

No comments:

Post a Comment