Swaum
ni kujizuia na kula na kunywa na vitu vinginevyo katika muda maalum kwa
nia ya kujikaribisha kwa Mwenyezi Mungu. Na ni moja wapo kati ya matawi
ya dini yaliyo ya lazima.
SWAUMU NA MASHARTI YA KUWAJIBIKA KWAKE
Ni wajibu kwa kila muislaam kufunga mwezi wa ramadhani yanapo kamilika mashartyi yafuatayo:
1-
Kubalehe, si wajibu kwa mtu ambae hajafikia balee kuanzia mwanzoni mwa
al fajiri ya mweziwa ramadhanikufynga, japo kuwa kauli ya ahwat inasema
ya kuwa ni bora kuitimiza ikiwa amenuwia kufunga sunna na akabalee kati
kati ya mchana.
2-3- Kuwa na akili
timamu na asiwe amezimia, ikiwa atapatwa na wazimu au kuzimia kiasi
kwamba nia izingatiwayo kwenye swaumu ikampita na akazindukana katikati
ya mchana haita kuwa ni wajibu kwake kufunga siku hiyo, ndio ikiwa
alitangulia kutia nia kabla ya kuzimia au kupatwa na wazimu kauli ya
ahwat ni kuwa itamlazimu kuikamilisha swaumu hiyo.
4-
Asiwe na hedhi wala nifasi, kwa hivyo basi si wajibu kwa mwenye hedhi
wala mwenye nifasi kufunga na haita swihi kwa watu hawa wawili funga
hata kama hedhi au nifasi hiyo itakuwa ilichukua sehemu fulani ya siku
(mchana).
5- Kutokuwa na madhara katika
funga, kama akiwa na ugonjwa na ikiwa atafunga ataweza kudhurika ima
kwa kuzidisha ugonjwa huo au kuchelewa kupona au kuzi kwa maumivu, na
hayo yote huangaliwa kiwango cha kawaida, na hakuna tofauti kati ya kuwa
na yakini juu ya kupatikana madhara hayo au kuwa na dhanna juu ya
kupatikana madhara na kuwa na ihtimali ipelekeayo kukubali kuwepo kwa
khofu itokanayo na vyanzo vya kiakili, katika mambo yote hayo si wajibu
kufunga, na ikiwa atafahamu ya kuwa hata pata madhara kwenye nafsi yake
lakini akaogopa madhara kwenye heshima yake au mali yake pamoja na
kutatizika katika kustahamili hali hizo haita kuwa ni wajibu kwake
kufunga, pia ikiwa atakuwa amesongwa na jambo la wajibu lililo sawa na
hilo au lenye umuhimu zaidi kama lau kama ataogopea heshima ya mwenziwe
au mali yake pamoja na kuwa ni wajibu wake kuihifadhi.
6-
Kutokuwa msafiri, lau kama atakuwa katika safari ambayo ni juu yake
kupunguza sala, haita kuwa wajibu kwake kufunga bali pia haiswihi funga
yake, ndio safari ambayo ni wajibu kukamilisha sala saumu haita anguka
yaani ni wajibu kufunga.
Mas’ala: Sehemu
ambazo msafiri ana hiari ya kupunguza au kukamilisha sala itamlazimu
sehemu hizo kula na swaumu haita swihi sehemu hizo.
Mas’ala:
Huzingatiwa katika kujuzu kula kwa msafiri kuwa awe amevuka mpaka wa
mji wake, mpaka ambao huzingatiwa katika kupunguza sala na ufafanuzi
wake umepita katika mas’ala ya sala ya msafiri.
Mas’ala:
ni wajibu –kwa kauli ya ahwat- kukamilisha funga kwa mtu ambae
amesafiri baada ya kupinduka kwa jua na swaumu hiyo itatosheleza
hakutakuwa na haja ya kuilipa, ama alie safiri kabla ya kupinduka jua
haiswihi kwake kufunga siku hiyo- japo kuwa atakuwa hakunuwia safari
kuanzia usiku kwa kauli ya ahwat- kwa hiyo inajuzu kwake kula (kuto
funga) baada ya kuuvuka mpaka wa mji wake na ni juu yake kuilipa swaimu
hiyo.
Mas’ala: Ikiwa masafiri atarudi
kwenye mji wake au kupita sehemu ambayo anakusudia kubakia hapo kwa muda
wa siku kumi kuna sura zifuatazo:
1- Arudi sehemu hiyo baada ya kupinduka kwa jua, katika hali kama hii si wajibu kwake kufunga.
2- Awe amerudi kabla ya kupinduka kwa jua na katika safari yake alikula, wakati huo si wajibu kwake kufunga pia.
3-Awe
amerudi kabla ya kupinduka kwa jua na awe hakula katika safari yake,
katika sura kama hii ni wajibu kwake kunuwia funga na afunge kwa muda
ulio bakia.
Mas’ala: ikiwa msafiri
atafunga kwa kuto fahamu hukumu na akafahamu hukumu hiyo baada ya
kumalizika mchana, funga yake itasihi na si wajibu kwake kuilipa na
ikiwa atafahamu hukumu hiyo katikati ya mchana saumu itabatilika na mtu
alie sahau saumu yake haita swihi.
Mas’ala:
Inajuzu kusafiri katika mwezi wa ramadhan hata kama si dharura, na
nilazima kuto funga katika safari hiyo, ama katika mambo mengine maalum
ya wajibu kauli yenye nguvu inasema haijuzu kusafiri ikiwa jambo hilo ni
wajibu kwa kuchukua malipo na mfano wake na vile vile siku ya tatu kati
ya siku za itikafu, ama kauli iliyo dhahiri ni kuwa inajuzu kusafiri
ikiwa wajibu huo ni kwa sababu ya nadhiri, ama yamini (kiapo)
kukiunganisha na hukumu hiyo kuna ishkaali.
Mas’ala:
Funga ya wajibu haiswihi kwa msafiri ambae katika safari yake ni wajibu
kupunguza sala- pamoja na kufahamu hukumu hiyo- isipokuwa katika sehemu
tatu:
1- kufunga siku tatu nazo ni
siku ambazo ni baadhi ya siku kumi ambazo zinakuwa badala ya hadyu
(mnyama katika hajji ya tamattui kwa yule ambae atashindwa kuitekeleza.
2-Kufunga siku kumi na nane ambazo ni badala ya mnyama ikiwa ni kafara kwa mwenye kutoka arafa kabla ya kuzama jua.
3-
Kufunga swaumu ya sunna ambayo imetiliwa nadhiri kuifungakatika safari
sehemu nyingine sawa iwe safari au nyumbani, kama ambavyo haiswihi
kufunga saumu ya wajibu safarini tofauti na sehemu zilizo tajwa, vile
vile haisihi kufunga saumu ya sunna isipokuwa siku tatu kwa ajili ya
hajja katika mji mtukufu wa madina na kauli ya ahwat ni kuwa iwe siku ya
juma tano, al khamisi, na ijumaa
Mas’ala:
Huzingatiwa katika kusihi kwa funga ya sunna ya kuwa mtu asiwe na dhima
ya kulipa funga ya mwezi wa Ramadhani, na hakuna madhara ikiwa atakuwa
na funga ya wajibu kwa kuchukua malipo au ya kulipa kadhaa au ya kafara
na mfano wa hizo, ikiwa anafunga hizo itajuzu kwake kufunga saumu ya
sunna katika sehemu zote hizo kwa kauli ya adh’har, kama ambavyo
inaswihi kwake funga ya sunna ambayo inaswihi kuifungia safarini hata
kama atakuwas na kadhaa ya mwezi wa Ramadhani kutokana na kauli ya ahwat
na inajuzu kwake kuchukua ujira kwa ajili ya kufunga swaumu ya wajibu
kwa ajili ya mtu mwingine au kumfungia kwa kujitolea kabla ya kulipa
swaumu zake za mwezi wa Ramadhani.
Mas’ala:
Mzee wa kiume na kike pindi ikiwawia vigumu kufunga inajuzu kwao kula
na badala yake watatoa kibaba kimoja cha chakula kila siku ikiwa ni
kafara ya siku hiyo, na si wajibu kwako kuilipa siku hiyo, na ikiwa
watashindwa kufunga basi funga itaanguka kwao na vile vile wakati huo
kafara itaanguka, na hukumu hii hutumika kwa mwenye kiu ( yaani mwenye
ugonjwa wa kiu) pia ikiwa funga itamtatiza atatoa kila siku kibaba
kimoja cha chakula na ikiwa hakuweza kutoa kibaba hicho pia uwezekano wa
kafara kuporomoka upo.
Mas’ala: mama
mja mzito ambae siku zake zimekaribia ikiwa ataogopa kupatwa na madhara
yeye mwenyewe au mwanae itajuzu kula- bali huenda ikiwa wajibu kama
ikiwa funga itamlazimu kupata madhara yaliyo haramishwa kwa mmoja kati
ya watu hao wawili- na atatoa kafara kila siku ya kibaba kimoja cha
chakula na ni wajibu kwake kuilipa funga hiyo.
Mnyonyeshaji
mwenye maziwa kidogo ikiwa ataogopa yeye mwenyewe kupatwa na madhara au
mwanae anae nyonya itajuzu kwake kula- bali pengine huenda ikawa wajibu
kama tulivyo sema katika mas’ala yaliyo tangulia- na ni juu yake
kuzilipa siku hizo na kutoa kafara kwa kila siku kibaba kimoja cha
chakula, na hakuna tofauti kati ya mnyonyeshaji sawa awe mama au mtu
alie chukua ujira kwa kazi hiyo au mwenye kujitolea kufanya kazi hiyo,
na kauli ya ahwat inasema ya kuwa ni lazima hukumu hii itumike pale tu
ikiwa njia pekee ya kunyonyesha ni hii na hakuna njia nyingine ya
kumnyonyesha mototo isipo kuwa hii hata kama ni kutumia njia nyingine
ikiwa hakuna kizuwizi, ama ikiwa kuna uwezekano huo haitajuzu kwake
kula.
Mas’ala: Kibaba cha chakula ni
sawa na kilo tatu takriban,na ni bora zaidi kiwe ni kibaba cha ngano au
unga wangano na kauli ya adh;har ni kuwa inafaa aina yoyote ya chakula
hata kama ni mkate.
No comments:
Post a Comment