Yeye ndie Imam na Al-hujjatul-mahdiy (a.s), Mohammad bin Hassan (a.s) na mama yake ni Sayyidah Narjis.
Alizaliwa (a.s) katika mji wa Samarraa usiku wa nusu ya mwezi wa Shaaban, mwaka (255) hijiria.
Na
yeye (a.s) ndio hoja wa mwisho wa Mwenyezi Mungu juu ya ardhi na
Khalifa wa mwisho wa Mtume (s.a.w) na Imam wa mwisho wa Waislaam, maimam
ambao ni kumi na mbili na Mwenyezi Mungu-kwa utashi wake-ameurefusha
umri wake mtukufu katika Dunia hii ili ardhi isibakie bila hujja wa
Mwenyezi Mungu, kwani kama kusinge kuwa na hujja basi ardhi inge didimia
pamoja na watu wake na yeye Imam haonekani kwa watu na Mwenyezi Mungu
atamdhihirisha katika Aakhiriz-zamani (Zama za mwisho) baada ya Dunia
kujawa na dhuluma na ujeuri (uovu), ili aijaze dunia hiyo kwa uadilifu
na usawa.
Hakika
Mtume (s.a.w) na maimam watwaharifu walitoa habari ya kuwa yeye atakuwa
na ghaibah (Atatoweka na kuto onekana) kwa muda mrefu, na hatakuwa
thabiti kwenye juu ya Uimam na wilaya yake na kumuamini isipokuwa yule
ambae Mwenyezi Mungu ameujaribu moyo wake kwa Imani, na katika siku za
ghaiba yake atakuwa katika hali ya kuwafikishia manufaa watu wa Ardhini
kama jua lifikishavyo manufaa na faida zake kwa watu hao hata kama
litakuwa limefunikwa na mawingu, na Mwenyezi Mungu atambakiza hai mpaka
utakapo fika wakati wa kudhihiri kwake, na hapo kudhihiri kwa idhini
yake Mwenyezi Mungu mtukufu na kuimiliki (kuitawala) Dunia yote na
kueneza uadilifu na usawa Duniani na kueneza Uislaam na misingi yake
yote na kuitekeleza Qur'ani na amri zake kwa watu wote na katika nyanja
zake zote za maisha, na hapo Kheri kuenea na saada kutangaa kwenye miji
yote na kuwaenea waja wote na kuthibitika kauli yake Mwenyezi Mungu
isemayo:
( ليظهره علي الدين كله ولو كره المشركون)
Ili auidhihirishe Uislaam juu ya dini zote hata kama washirikina watachukia.
Ewe
Mwenyezi Mungu harakisha faraja yake na kufanye kwepesi kudhihiri kwake
na utujaalie tuwe miongoni mwa wasaidizi na answari wake.
No comments:
Post a Comment