UTANGULIZI
KWA JINA LA ALLAH SWT MWINGI WA
REHEMA MWENYE KUREHEMU.
Natoa shukurani zangu kwa Allah swt, Mtume Muhammad s.a.w.w. pamoja na
Ahli Bayt tukufu ya nyumba yake a.s. kwa kunijaalia uwezo wa kuandika makala hawa.
Allah swt amewatuma Mitume a.s. kuja kutuongoza na kutuletea maamrusgo
Yake ili tusihangaike kwa kutapatapa huku na huko tukitafuta kipi ni kweli na
sahihi. Lakini wapo watu wenye uchu wa kujitakia dunia kwa hali yoyote ile,
hivyo wanawasahau Mitume a.s. na ujumbe waliokuwa wametuletea katika miaka yote
hiyo. Kwa tamaa na uroho wao wanachafua dunia na desturi za amani.Wanawatesa na
kuwateketeza watu bila ya kujali kuwa wao wafanyavyo si haki.
Mtume s.a.w.w. alisema kuwa, “Ummah wangu utagawanyika katika makundi
sabini na tatu, ni kundi moja tu litakaloingia Peponi.” Hivyo makundi sabini na
mbili, kama zilivyobainishwa, zitaingia Motoni kwa sababu za itikadi zao
potofu, na kwa hakika hayo yameshakwisha tokea. Makundi haya sabini na mawili si
makundi ya makafiri kwa kutojua ilimu sahihi ya Qur’an na Hadith, lakini
wataingizwa Motoni kwa sababu wao wamediriki kuubadilisha Uislamu. Na hao wanaitwa ahlul bidaa au -dalala
wakaidi. Wakaidi, kwa sababu wao ni Waislamu, na hapo mbeleni watatolewa kutoka
Jahannam na kupelekwa Peponi. Mbali na hao, wapo wale ambao ni Waislamu lakini
wanakuwa katika jitihada za kuubadilisha kwa ilimu yao potofu na kipeo chao
kidogo, hivyo wanatoka nje ya Uislam. Kwa hakika hao watabakia Motoni kwa
milele. Nao ni Zindiq na wachafuzi.
Leo, watu waitwao la-madhhabi wanatumia mamilioni ya madola kwa
kueneza imani zao potofu katika kila nchi humu duniani. Ni jambo lakusikitisha
mno kuona kuwa hawa waroho wa mapesa wamekuwa wakivutiwa mno katika imani zao
potofu na za kufitini, huku nyuma wakiachia hazina kubwa waliyoachiwa na Ahl
al-Bayt a.s. ya Nyumba ya Mtume Muhammad s.a.w.w. na Maulamaa wa Ahl-as-Sunna.
Hao Mawahhabi wamejaribu kwa jitihada zao zote kuwadanganya Waislamu kuwa
vitabu vya Maulamaa wao vinawapotosha. Wao wametayarisha vitabu na propaganda
zao dhidi ya Islam halisi iliyokuja kwetu kutokea Mtume Muhammad s.a.w.w., kwa
maandiko ya Mawahhabi yaliyojaa upotofu na vitisho na ulaghai.
Kwa hakika Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab na kizazi chake wamekuwa
wakitoa imani zao potofu kwa kuchapa vitabu ambavyo vimekuwa vikiwapotosha
Waislamu kwani walikuwa wakizitumia Ayah za Qur’an tukufu dhidi ya Waislamu
wenyewe. Wao hata walithubutu kuwaita Waislamu kuwa ni Makafiri kwa kuelezea
kiuongo Ayah na Hadith. Na jambo hili ndilo limenifanya mimi niandike mfululizo wa makala hizi ambazo zitafichua uasili wao.
Mada hizi ni sehemu moja ya kitabu kamili
juu ya Mawahhabi. Sehemu hii inazungumzia vile Mawahhabi walivyotokezea, vile
walivyo enea vile majahili na makatili waliojiingiza katika Uwahhabi ili
kujipatia mali na vyeo wamewateketeza na kuwaua Waislamu na kuzipora mali zao.
Tunamwomba Allah swt awasaidie Waislamu wasiteleze kutumbukia katika
mitego ya Mawahhabi.
No comments:
Post a Comment