Katika mwaka 1306 (1888) wakati ambapo kitabu kiitwacho Mir’at al-Haramain kilipoandikwa,
kiongozi wa Najd alikuwa ‘Abdullah ibn Faysal, kutokea kizazi cha Muhammad ibn
Sa’ud, na Qadhi pia alikuwa ametokana na kizazi cha Muhammad ibn ‘Abd
al-Wahhab.
Baba yake mzazi wa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab, ‘Abd al-Wahhab, ambaye
alikuwa ni mcha Mungu, ‘alim halisi katika Madina, ndugu yake Sulaiman ibn ‘Abd
al-Wahhab na waalimu wake walikuwa wamekwisha tambua kutoka maneno, matendo,
ishara na mawazo yake, ambayo mara kwa mara alikuwa akidhihirisha katika sura
ya maswali alipokuwa mwanafunzi huko Madina, kuwa atakuwa mpotofu ambaye
ataidhuru mno Islam kwa undani katika kipindi kifupi kijacho. Wao wote kwa pamoja
walimuasa na kumnasihi aache mawazo yke hayo ya upotoshi na vile vile walikuwa
wakiwashauri Waislamu wote kwa ujumla wasimfuate na wajiepushe na Muhammad ibn
'Abd al-Wahhab. Lakini katika muda mfupi tu walikumbana na jambo walilokuwa
nalo khofu, na yeye alianza kueneza uzushi wake huo kidhahiri kwa jina la
Uwahhabi. Kwa ajili ya kuwapotosha majahili na wapumbavu, yey alijitokeza kwa
mawazo ya kurekebisha na kuzua mambo ambayo hayakubaliani na vitabu vya
maulamaa wa Islam. Yeye alithubutu kwa kishindo kuwatuhumu Waislamu wa Ahl
as-Sunnah wal Jama’a kuwa ni makafiri. Yeye alikuwa akiamini kuwa ni shirk kumwomba Allah swt kwa kupitia
Mtume Muhammad s.a.w.w. au Mitume mingine a.s. au ma-Awliya’’
na kuzuru makaburi.
Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab alikuwa akimwona mtu yeyote yule anayesali
na kuomba karibu na kaburi kuwa ni Mushrik.
Yeye alisisitiza kuwa Waislamu wasemao kuwa mtu fulani au kitu fulani mbali na
Allah swt kimefanya hivi au vile,kwa mfano, kwa kusema kuwa dawa fulani na fulani zimeponyesha au mimi nimeweza kupata kile nilichokuwa
nikihitaji kwa kupitia Wasila wa
Mtume Muhammad s.a.w.w. au au mawali
fulani fulani basi hao wote ni Mushrik.
Ingawaje waraka wa Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab hazikuwa chochote isipokuwa ni
uongo na fitina tu, lakini majahili hawakuweza kutofautisha baina ya ukweli na
uongo, wale wasiokuwa na kazi, wazururaji, majahili, wenye kuvizia bahati na
wenye nyoyo ngumu walizipokea mawazo yake na kujiweka bega kwa bega pamoja naye
na kuamini wale Waislamu waliokuwa katika njia sahihi kuwa wote kwa pamoj ni
makafiri.
Wakati Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab alipowaomba ruhusa watawala wa
Dar’iyya kutaka kueneza imani zake za uzushi kwa kupitia utawala wao, wao
walimpokea kwa mikono miwili kwa matumaini ya kupanua eneo la utawala na kuzidi
kwa nguvu zao. Wao walijitolea kwa hali
na mali kueneza imani hizo kila mahala.
Wao hata walithubutu kutangaza vita dhidi ya wale wote waliokuwa
wakimkataa na kumpinga. Watu Mahayawani
na wateka nyara wa jangwani walikuwa
wakishindana katika kujiunga na jeshi la Muhammad ibn Sa’ud wakati pale
iliposemwa kuwa ni halali kumwua na kupora mali za Waislamu. Katika mwaka 1143
( 1730 ), Muhammad ibn Sa’ud pamoja na Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab
wakishirikiana kwa pamoja walifikia maafikiano kuwa wale wote ambao hawata
kubalia Uwahhabi, basi watakuwa ni makafiri na Mushrik, na hivyo ilikuwa ni halali kwao kuwaua na kutaifisha mali
yao yote, na walitangaza rasmi amri hiyo miaka saba iliyofuatia. Hapo ndipo Muhammad ibn 'Abd al-Wahhab
alipoanza kutunga uzushi wa ijtihad
pale alipokuwa na umri wa miaka thelathini na miwili na aliitangaza kidhahiri
pale alipokuwa na umri wa miaka arobaini.
No comments:
Post a Comment