Thursday 5 July 2012

Nimevaa hijabu ili niwe karibu na Mwenyezi Mungu


 Nimevaa hijabu ili niwe karibu na Mwenyezi Mungu
Masha baada ya kukubali Uislamu alikuwa ni Mwanamke wakirusia, Muimba Muziki, Mshiriki wa Model wa Dunia kukubali Uislamu.
Ripoti ya ABNA- Na haya ni mazungumzo yaliofanyika baina ya Mwandishi wa habari na Masha;
-ikikuwaje kukubali Uislamu?
Masha: Mwanyezi Mungu kanisaidia katika hilo na huu ni uwezo wake Allah.
-kipindi ulichokua Muimba Muziki je ulifikiria kama Siku moja utakuwa Muislamu?
Masha: la hasha Sikufikiria hata kamwe kama inaweza kutokea kuwa Muislamu.
-Je kunanjia zozote zile ulizopitia katika kusaidia kuwa Muislamu?
Masha: nilipo kuwa Muislamu nilikuwa na Rafiki yangu alitokewa na matatizo na kuwekwa katika komaa (kutozungumza au kusema au harakati yoyote ile) nilifikiria njia ya kumsadia Rafiki yangu ni kumuombea Dua ni swali na kumuomba mola amsadie Rafiki yangu baada ya Dua yangu alipona na kunipigia Simu na kunieleza kuwa mimi ndie niliemsaidia kupona katika Maradhi yake, tokea kipindi kile nilibadilika na kuwa tofauti.
-unakazi gani kwa sasa?
Masha: sasa ni Mwalimu wa Chuo kikuu.
-Je hadi sasa bado unasikiliza Muziki?
Masha: Ndio bado nasikiliza Muziki  wa kundi la Raihan kundi la Sami Yusuf.
-Je unapoangalia Picha zako katika Internet haukasiriki?
Masha: mie mwenyewe sitaki kuona Picha hizo ila si vibaya Watu wazione na kuzingatia kuwa kuna uwezekano wa kuzaliwa mara ya pili na kufikiria machafu tuliyo fanya hapo kabla.
-Ni kitu gani unaweza kuwambia Watu kunako Uislamu?
Masha: Uislamu unasema; ni lazima kumjua Mwenyezi Mungu  na kama hatutoweza tujitahidi kumjua ili kuondokwa na Madhambi, Kiburi, Husda n.k.
-Ama kwa wasio kuwa Waislamu utawaambia vipi?
Masha: kwa wale bado hawajakuwa Waislamu wajitahidi kujua haki na kuacha Imani za ujinga
 

No comments:

Post a Comment