Sunday 1 July 2012

WAPIGANAJI WA KIISLAMU WABOMOA KABURI LA IMAMU TIMBUKTU

Wapiganaji wa Mali waitwao Answar diini wanaoshikilia eneo kubwa la kaskazini ya nchi hiyo wameanza kubomoa makaburi ya viongozi wa kiislamu katika mji wa Timbuktu. Mji huu ni maarufu Afrika kwa Historia ya Uislamu tokea kale na waislamu wanauita mji wa mawalii 333. 

Wapiganaji hao wameanza kwa kubomoa kaburi la Imamu Sidi Ibrahim kwa madai kwamba ni ukafiri kujengea makaburi. Hii sio mara ya kwanza kwa wapiganaji wanaodai kuwa ni wa kiislamu kubomoa maeneo matukufu ya kiislamu. Watu wa aina hii wamewahi kuboa makaburi katika miji ya Makka na Madina ambako ndiko chimbuko la uislamu. Tafadhali fuatilia historia ya makaburi ya Madina yaitwayo Baqii.

Tabia ya kubomoa maeneo matakatifu ya kiislamu haikubaliki hata kidogo. Uislamu umewaagiza waislamu waheshimu vitu vitakatifu kama Qur'an, misikiti, makaburi na hata watu wote na ubinadamu kiujumla. 

kwa mfano Mtume Mohammad alikuwa akisimama kila alipoona jeneza likipita mbele yake kwenda mazishini, lakini pia alikuwa akisimama kila alipopata mgeni ili kumlaki na hata alipokuwa akitembelewa na watu wasiokuwa waislamu alisimama kuwalaki. 

Lakini watu hawa wanabomoa sio makaburi tu bali hata misikiti. Misikiti imekuwa ikilipuliwa kwa mabomu katika maeneo mengi ya dunia na watu hawa kama vile Pakstani, India, Yemen, Syria, Uturuki na iraq. Kwa kuwa Uislamu unahimiza heshima kwa kila mtu aliyehai au aliyekufa, hauwezi kuagiza waumini wake kuvunja makaburi ya maumini wengine.

Hiki kikundi cha Anwari diini na vingine vyenye misimamo ya ajabu ajabu kama Boko Haram ni vikundi vilivyoanzishwa kwa msaada ya mashirika ya kijasusi CIA la Marekani na MOSSAD la Israel ili kuwachanganya waislamu washindwe kujua ukweli uko wapi juu wa Uislamu? Na watu washindwe kujua Uislamu sahihi kwani vijana wengi wanapenda vurugu?



No comments:

Post a Comment