SHIA NA QUR’AN TUKUFU
Shia wanaitakidi kuwa Qur’an ni wahyi wa Mwenyezi Mungu
uliteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika ulimi wa Nabii mtukufu kwa
kubainisha kila kitu, nayo ni muujiza wa milele ambao wanadamu wameshindwa
kupambana nao katika balagha, fasaha na katika ukweli na maarifa ya hali ya
juu, haiguswi na mabadiliko, mageuzi wala upotovu, na hii ambayo iko mikononi
mwetu tunayoisoma ndio ile ile Qur’an iliyoteremshwa kwa Nabii (s.a.w.w.) na
atakaye dai yasiyokuwa hayo basi ni muongo au ni mwenye kukosea au
amechanganyikiwa na wote hawako katika uongofu, hakika hayo ni maneno ya
Mwenyezi Mungu ambayo hayapatwi na upotovu kwa hali yeyote.
Sheikhul Muhadithiina Muhammad bin Ali Al-Qummiy ambaye amepewa
lakabu ya Asuduuq amesema: Itikadi yetu katika Qur’an ambayo ameiteremsha
Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Nabii wake Muhammad (s.a.w.w.) ni ambayo iko baina
ya jalada mbili na ambayo iko kwa watu na sio zaidi ya hayo... na
anayetunasibishia kuwa tunasema zaidi ya haya basi ni muongo.
Assayid Al-Khuiy ambaye ni mmoja wa marajii wakubwa wa kishia
katika zama hizi anasema, “iliyomashuhuri baina ya Waislamu ni kutokuwepo
opotoshaji katika Qur’an na iliyopo mikononi mwetu ni Qur’an yote iliyoteremshwa
kwa Nabii (s.a.w.w.).
Ama Sheikh Muhammad Al-Ghazaaliy anasema katika kitabu chake Difau
anil-aqiydati wa shariah dhidu matwa’inil-mustashiriqiyna “Nimesikia kutoka kwa
hawa miongoni mwa watu ambaye anasema katika majilisi za hadhara: Hakika Shia
wana Qur’an nyingine ambayo ni zaidi na inapunguza Qur’an yetu iliyo maarufu
nikamwambia: Iko wapi hii Qur’an? na kwa nini majini na wanadamu hawakuona
nakala yake kwa muda wote huu mrefu? Huu uongo ni wa nini?... kwa nini
kusingizia wahyi na watu. Ama hadithi ambazo sio
sahihi ambazo baadhi wanaweza kuzitegemea ambazo zinaeleza kupotoshwa kwa
Qur’an na ambazo zipo katika vitabu vya hadithi katika Shia, hakika ni dhaifu
na hazikubaliwi na mfano wake ni nyingi katika vitabu sahihi vya Ahlus-Sunna na
tutaonyesha mifano ya hayo katika Sahih Bukhariy, tunatanguliza hadithi
walizozipokea kuhusu kusahau Mtume (s.a.w.w.) katika baadhi ya Aya:-
Kutoka kwa baba yake kutoka kwa Aisha amesema: Mtume wa Mwenyezi
Mungu alimsikia mwanaume anasoma sura usiku akasema! Mwenyezi Mungu amrehemu
amenikubusha Aya kadha wa kadha nilikuwa nimezisahau katika sura kadha wa
kadha. Vile vile katika Sahih Bukhariy ni kwamba,
walipokuwa wanakusanya Qur’an hawa kupata sehemu ya Surat Tauba isipokuwa kwa
Khuzaimah Al-Answariy na hii inapingana na ukweli unaosema kuwa Qur’an
imepokewa kwa Tawatiri na wala sio kwa Riwaya za Ahadi (mtu mmoja):
Al-ahzaab nilikuwa namsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.)
anaisoma usiku kucha isipokuwa kwa mtu mmoja Khuzaimah Al-Answariy Khuzaima
Al-Answariy ambaye Mtume wa Mwenyezi Mungu amejaalia ushahidi wake kuwa ni sawa
na ushahidi wa waumini wawili.
Nilifuatalia kukusanya Qur’an kutoka kwenye vipande vya nguo,
mifupa, magome kwa watu waliohifadhi hadi nikakuta Aya mbili za sura ya Tawba
kwa Khuzaimah Al-Answariy na sikuipata kwa yeyote asiyekuwa yeye.
Haya ni maelezo ya wazi kuwa Mashia tunaamini kuwa Qur’an
tuliyonayo ni kamilifu kama ilivyoshuka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Na hadith
zinazodai kuwa Qur’an ni pungufu au zaidi ni dhaifu na za uongo na zinapatikana
zaidi katika vitabu vya Ahlulsunah waljamaa kuliko katika vitabu vya Shia. Hivyo
tusisingiziane imani mbovu ili tu kuzua mtafaruku au kuzuia watu wasijue
ukweli.