KIINI CHA MACHAFUKO KATIKA
UISLAMU
Mpaka katikati ya karne ya
kumi na saba (17) Uislamu ulikuwa na nguvu kubwa za kisiasa duniani. Nguvu hii
ilitokana na mwenendo wa Serikali ya Wauthman (Dola ya Wauthmani) ambayo
ilikuwa imetawala eneo kubwa la Afrika Kaskazini, Bara Arab, nchi za Ulaya
Mashariki kama vile Bulgaria, Hungaria, Yugoslavia, Romania, na hata sehemu za
Urusi n.k.
Lakini watawala wa mataifa
ya Kikristo, hususan wa Ulaya Magharibi, walipoona Uislamu unazidi kuenea na
kupanda mbegu safi ya utamaduni wake, wakaona vibaya kwa kuwa mwenendo wa
Kiislamu una nguvu kubwa na ni vigumu
kuwafanya watu kubadilika baada ya kuingiwa na silika ya Kiislamu. Kwa
haraka kabisa wakaunda vikundi vya wataalamu
mbali mbali vikiongozwa na Serikali zao kuzunguka katika mataifa ya Kiislamu
kwa nia ya kutafiti njia itakayowasaidia kuondoa mshikamano wa Waislamu.
Maadui walifanya uchunguzi kwa uyakinifu na wakabainikiwa kuwa
nguvu za Waislamu hutokana na umoja wao ambao kwa hakika ndio msingi wa
mafanikio ya kila tabaka. Pili, ni kuwa waliona wazi kuwa Waislamu ni wenye
kujenga tabia ya kuaminiana wao kwa wao, kwa hali hiyo isingekuwa rahisi
kuwaingia na kuwasaliti.
Hatua ya kwanza ikawa
kupenyeza baadhi ya watu wao ndani ya Waislamu na kujifanya Waislamu kusudi
wapate imani ya Waislamu.
Hatua iliyofuatia ilikuwa ni
wao kuingia katika vyeo vya Kiislamu na kujifunza elimu humo. Inaripotiwa kuwa
Napoleon alifika Misri na kujifunza
katika kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Al-Azhar.
Vikundi vingine
vilijihusisha na kutafiti njia za kuingia
ukoloni katika maeneo ya Kiislamu na kuziangusha Serikali zake. Waitaliano
waliingia Libya na kuanzisha utawala wao
huko. Waingereza waliuangusha utawala wa Tippu Sultan mwaka 1799 na kuondolea
mbali matumaini ya kisiasa ya Waislamu
katika Bara Hindi. Kuanzia hapo Ubeberu wa Kiingereza ulitashahari katika eneo
hilo. Katika miaka ya 1894 Waingereza walifanikiwa kuwapata vibaraka ambao walijitolea kuutumikia utawala
wao dhidi ya Uislamu. Ghulam Ahmad wa Kadian
akaunyenyekea Ukafiri wa Kiingereza kufikia hadi ya kusema baada ya
kumwamini Mwenyezi Mungu imani ya pili
ni kumwamini Malkia.
Uturuki nako Serikali
iliangushwa. Hii ilikuwa baada ya vibaraka kuingia katika ngazi za juu katika Serikali.
Adhana ilipigwa marufuku baada ya mapinduzi. Katika utaratibu huu maadui wa
Uislamu waliweza kufanikiwa kuuvunja
umoja wa Waislamu kwa kuwatumia
wanachuoni na watu maarufu katika wenye
tamaa. Na huo basi ulikuwa mwanzo wa machafuko. Mpaka hivi sasa, na katika kila
nchi zenye Waislamu na ambazo zinatawaliwa na watu wenye nia mbaya na Uislamu,
wanawatumia Waislamu wenye mawazo ya kitumwa.
Miongoni mwa watu
waliotumiwa kuvunja nguvu za waislamu kwa kuanzisha vita vya wenyewe kwa
wenyewe katika kila kona ya bara Arabu alikuwa Muhammad Abdulwahhabi
akishirikiana na mfalme wa Najdi, kazi ambayo wafuasi wake wanaendelea nayo
mpaka sasa. Kila eneo lenye Mawahhabi amani imetoweka, anzia Urusi, Pakistan,
Afghanistan, India, China, Iran, Iraq, Yemen, Kuwait, Saudi Arabia, Syria,
Misri, Libya, Tunisia, Somalia, Lebanon, Jordan, Morocco n.k. kote kuna matukio
yametokea ya kuwalipua na kuwashambulia watu wasiokuwa na hatia kwa madai tu ya
kutetea madhahebu yao au kupambana na makafiri, cha ajabu utakuta wanaoitwa
makafiri ni waislamu wenzao wa kishia na kisunni.
No comments:
Post a Comment