HAWA NDIO WATU WALIOUPINGA
UKHALIFA BANDIA WA ABUBAKAR SIDIQ (R.A)
Ndani ya Uislamu uchaguzi sio
kitu kinachopokelewa vizuri lakini baada ya Mtume kufariki, waroho wa madaraka
walikutana katika ukumbi iitwao Saqifatu bani Saida na kufanya uchaguzi mbovu
kuliko chaguzi zote duniani, ambapo Abubakr alichaguliwa kwa kutumia upanga wa
Umar bin Khatab ambaye alitangaza katika ukumbi huo kuwa Khalifa ni Abubakar na
yeyote atakayepinga atakamkata kichwa. Waislamu kwa woga walikubali utawala huo
wa kibabe na ukatili mkubwa.
Lakini Masahaba majasiri
walipinga, miongoni mwao wakiwa Mashia ambao walikuwa wakiitwa Mashia wa Imam
Ally (a.s).
Historia inaonesha kuwa baadhi
ya wapingaji hao ni Bwana mkubwa wa Kiansar Saad bin Ubbadah na mwanawe Qais
bin Saad, Ali bin Abi Talib, Zubair bin Al-Awwam,[1] Abbas
bin Abdil-Mutalib, Bani Hashim wengine na baadhi ya Masahaba ambao walikuwa
wakiona kuwa Ukhalifa ni haki ya Ali (a.s.) na walipinga baia hiyo na wakabakia
nyumbani kwa Ali mpaka wakatishiwa kuchomwa moto.[2]
REJEA
[1]-Sahih
Bukhar Juz. 8 uk. 26 Babu Rajmil-Hubla Minaz-zina.
[2]--Tarikhul-Khulafai
cha Ibn Qutaibah Juz. 1 uk. 18
Kwa kulinganisha hayo tunaona
Mashia wanathibitisha kinyume cha usemi wa Masunni na wanasisitiza ya kwamba
Mtume (s.a.w.) alimbainisha Ali kuwa ni Khalifa na akatamka hili katika matukio
mengi na lililo mashuhuri ni lile la Ghadir Khum.
No comments:
Post a Comment