Saturday, 19 September 2015

FUNDISHO KUTOKANA NA KIFO CHA MIRZA TAHIR QADIAN, IMAM WA JUMUIYA YA AHMADIYA.

FUNDISHO KUTOKANA NA KIFO CHA MIRZA TAHIR QADIAN, IMAM WA JUMUIYA YA AHMADIYA.

Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh.
Imam wa Jumuiya ya Ahmadiya, Mirza Tahir Qadiani afariki dunia. Yule aliyeitwa Imam na Khalifa wa Kujitawaza wa Jumuiya ya Ahmadiya, Mirza Tahir Ahmad Qadiani alifariki duniya mnamo Aprili 19 2003. Kila mtu lazima afe siku yake ikifika, lakini vifo vingine ni fundisho kwa wengine. Mnamo mwaka 1988 Mirza Tahir Ahmad alitoa chagizo la Mubahila (dua ya maapizano) kwa Umma mzima wa Waislamu, akiwaita makafiri na waongo. Changamoto hii ya Mubahila ikamuelemea Mirza. Ilimtia matatani na kumuweka katika hali ngumu ambayo hakuweza kujinusuru nayo kamwe na hatimaye ikamtowa uhai.


Baada ya kutoa changamoto hii, Mirza aliishi kwa kujificha lakini wanazuoni wa kiislamu wakayafanya maisha yake yawe ya moto kwa kumchagiza mara kwa mara kufanya naye dua ya maapizano. Wanazuoni wengi waliikubali changamoto yake na wakamwita katika duwa ya ana kwa ana ya maapizano (kama ilivyokuwa Sunna ya Mtume Muhammad (s.a.w).

Said Abdul Hafiiz Shah aliyeanzisha harakati dhidi ya Ahmadiya mwaka 1991, naye pia aliikubali changamoto ya mubahila (dua ya maapizano) lakini Mirza Tahir hakuwa na ujasiri wa kukabiliana na yeyote katika dua ya maapizano. Kutokea kwenye jukwaa la harakati dhidi ya ahmadiya, waislamu wakamchagiza Mirza kufanya naye Mubahila katika miaka ya 1994, 1995, 1997, 1998 na 2000, lakini Mirza Tahir alipiga kimya kiasi kwamba alishindwa hata kulijibu tu chagizo hilo achililia mbali kulikubali.

Sheikh Manzoor Ahmed Chinioti amekuwa akienda London kila mwaka tangia mwaka 1989 na amekuwa akimchagiza Mirza kujiapiza kwamba yeye (Mirza Tahir) hakuwahi kufanya mambo ya kishoga (ubaradhuli). Ni muhimu kukumbuka kuwa baba yake Mirza Tahir, Mirza Bashiruddin Mahmud, Khalifa wa pili, alikuwa mzinzi, Muhuni, baradhuli wa kutupwa ambaye hakuacha kumpitia hata binti yake wa kuzaa na hakuwaacha hata ndugu zake ambao kwa sheria ya dini ya ufunuo, ni haramu hata kuwaoa.
Lakini wapi? Mirza Tahir amebakia kujificha nyumbani kwake Gressenhall. Mfuwasi wa zamani wa Ahmadiyya, Ahtesham-ul-Haq Abdul Bari, anayejishughulisha na harakati dhidi ya Ahmadiyya/Kadiyani mjini Mumbay, naye pia ametoa changamoto za mara kwa mara za Mubahila ambapo mwaka 1995 alikwenda hadi kwenye makao makuu ya Ahmadiyya mjini London kwaajili ya kufanya maapizano ya ana kwa ana na Mirza Tahir ambaye alikataa kumpa nafasi hiyo.
Lakini hatimaye Mirza Tahir alifanya kosa baya sana la kukubali changamoto ya duwa ya maapizano (japo si ya ana kwa ana).

Mnamo Juni 3 1999 duwa ya maapizano iliafikiwa baina ya bwana Illias Suttar wa Karachi na Murabi wa Qadiyani wa Karachi bwana Mohammed Othman Shahiid. Msingi wa maapizano haya ulikuwa ni ile changamoto ya mubahila aliyeitowa Mirza Tahir mwaka 1988. Mashahidi watatu kutoka kila upande walishuhudiya tukio hili la kihistoriya. Mnamo Julai 30 1999, mbele ya wajumbe 18.500 wa Kadiyani waliotoka sehemu mbali mbali ulimwenguni ambao walijumuika kwa ajili ya mkutano wa mwaka (Jarsa Salana) mjini London, Mirza Tahir alitamka hadharani kuikubali changamoto hii ya Illias Suttar na kusema: "Mungu atamuadhibu mtu muongo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Hata kabla ya mwangwi wa maneno yake haujamalizika, kweli muongo akatiwa mkononi na Mungu. Mnamo Agosti 20 1999 wakati Mirza Tahir alipokuwa akitowa Hotuba ya Ijumaa nchini Norway, ghafla alipigwa na kiarusi kilichomfanya aseme maneno yasiyoeleweka. (Ambacho kilisababisha hotuba yake ivurugike na kutoeleweka).
Haraka haraka akakimbiziwa London ambako alikaa ndani kwa takriban mwezi mzima. Mnamo Septemba 10,1999 alitoa hotuba ya dakika kumi ambapo alikiri kuwa alipatwa na ugonjwa wa akili ambao ulimfanya ashindwe kujielezea na hiyo ndiyo sababu iliyomfanya asionekane hadharani. Siku hiyo hakuweza kuongoza sala na badala yake Imamu akawa Ataul Mujiib Rashid. Kwa kipindi fulani baada ya hapo alikuwa akionekana kufanya makosa ya mara kwa mara katika hotuba na sala, wakati mwingine akimaliza sala baada ya rakaa moja tu.
Adhabu hii ya Mungu ilidhihirisha mbele ya macho ya walimwengu kuwa Mirza Tahir pamoja na Mirza Gulam Ahmadi Kadiyani walikuwa waongo.

Illias Suttar bado yu hai na bukheri wa afya hadi leo. Jumuiya ya Ahmadiyya imepiga kimya cha jumla juu ya swala hili la Mubahila ya Illias Suttar. Ndani na nje ya jumuiya hiyo, mara kwa mara watu wamekuwa wakiuliza: " Ni nani mshindi wa Mubahila? " Lakini Mirza Tahir naye amenyamaza kimya juu ya swala hili na hakutowa tamko lolote rasmi hadi mwisho wa uhai wake.

kutokana na tukio hili tunajifunza kwamba tusing’ang’anie imani zetu hata kama ni potofu bali tuwe tayari kubadilika pale ukweli unapotudhihirikia. 

No comments:

Post a Comment