IDADI NA
WAKATI WA SALA ZA FARADHI
Ujue kuwa
sala za Wajibu za siku zote ni tano:-
{a} Sala ya Asubuhi ni Rakaa mbili.
Na
nyakati zake ni Alfajir kabla ya kuchomoza jua.
{b} Sala ya Adhuhuri ni Rakaa nne: na {c} Sala ya Alasiri ni Rakaa
nne.
Na
nyakati zake sala hizi mbili ni dhuhuri hadi kuchwa jua.
{d} Sala ya Magharibi, nayo
ni Rakaa tatu, na {e} Sala ya Isha nayo ni Rakaa nne.
Na
nyakati zake sala hizi mbili ni magharibi hadi nusu ya usiku.
Hii ni
kwa mwenye kuwa mkazi wa mji au kama mkazi wa mjini. Lakini msafiri husali sala
za rakaa nne {Adhuhuri, alasiri na Isha} kwa rakaa mbili mbili kama sala ya
Asubuhi.
No comments:
Post a Comment