SIDDIQ (WAKWELI) NI WATATU
TU, KATIKA UISLAMU
Imam Muhammad ibn Ismail
al-Bukhari katika kitabu chake Tarikh al-Kabeer, ametaja maneno ya Mtume wetu
(s.a.w.w.) yalioelezwa na Ibn Abbas kuwa watu watatu ni “Siddiq”: hakika bila
shaka Hizqil mwamini kati ya watu wa
Firauni, Habib al-Najjar mwamini kati ya ukoo wa Yaseen na Ali Ibn Abi Talib
ndio wa kweli.
Nawab Siddiq Hasan Khan wa
Bhopal katika kitabu chake cha tafsir
kiitwacho Tafsir Fathul Bayan ameeleza hadithi kutokana na Ibn Abi
Laila, na hadithi hiyo hiyo imetolewa na Tafsir Durr-e-Manthur ya Jalaluddin Suyuti lakini iko tafauti ya
baadhi ya maneno tu, wanasema kwamba “Ni
watukufu watatu tu ambao hawakukufuru au
kumuasi Mwenyezi Mungu kabisa hata kiasi cha kupepesa macho na walikimbilia kuamini dini ya haki. Miongoni
mwao na wa mwanzo na bora wao ni Ali Ibn Abi Talib; wa pili mwamini katika
kaumu ya Firauni, na watatu wao anatokana na ukoo wa Yaseen. Na watatu hawa tu
ni Siddiq (Washuhudiawo na kweli).”
Wa kweli au Siddiq hapa
inakusudiwa, ni watu wa mwanzo kusilimu katika kaumu yao na tena hawakuwahi
kufanya dhambi, bali walipousikia Ukweli wa Uislamu waliupokea mara moja bila
kusita na wakaufuata moja kwa moja bila kuchanganya na mila zao zingine.
Nakuombeni tufuate nyendo
zao, nasi tuingie katika Uislamu moja kwa moja bila kuchanganya na mila zingine
za ajabu ajabu.
No comments:
Post a Comment