KUUMBWA KWA MWANADAMU
Hatua ya awali ya
uumbaji, pale ambapo Adam aliumbwa tunamwachia Allah.
Lakini kwa sasa hatua
ya kwanza katika kuumbwa kwa Mwanadamu hurejea kwenye hali wakati Kijusu
(Mimba) kinapowekwa kimpango katika tumbo la uzazi, ingawa imefungwa ndani ya
aina tatu za sitiri zilizo wazi na aina tatu za viza. Ya kwanza ikiwa ni ile ya
ukuta wa nje, ya pili ni ya tumbo la uzazi na ya tatu ni ya Kondo la nyuma. Huu
ni wakati ambapo kijusu hakiwezi kujilisha wala kuondoa madhara yoyote yatokanayo
nayo.
Mtiririko wa Hedhi
umeadilishwa ili kutoa lishe kwa ajili yake, kama vile maji yanavyochukua lishe
kupeleka kwenye mimea. Hivyo mpango huu huendelea mpaka kufikia wakati ambao
viungo vyake vimekamilishwa, ngozi juu ya mwili wake huwa imara kiasi chakustahimili
hali ya hewa - hivyo kwamba haiwezi kupata madhara yoyote kutoka kwenye hewa na
macho yake yanapata uwezo wa kustahimili mwanga.
Wakati vyote hivi
vinapokuwa vimekwisha fanyika, mama yake hupata uchungu wa uzazi, ambao kwa
ukali humtikisa kumfikisha kwenye kuhangaika, kufikia upeo wa kuzaliwa mtoto.
Na kwa kuzaliwa
mtoto, mtiririko wa heidhi uliokuwa ukipeleka lishe kwenye tumbo la uzazi
unabadilishwa kwenda kwenye matiti ya mama.
Ladha yake
inabadilishwa hivyo hivyo na rangi yake, na kuwa lishe aina ya pekee tofauti
ambayo hufaa hasa kwa hali ya mtoto, kama na wakati ahitajiayo (hayo) hayo,
kulinganishwa na mtiririko wa damu.
Wakati ule ule wa
kuzaliwa kwake anaanza kutikisa na kulamba midomo yake kwa ulimi wake kuonyesha
hamu yake ya (kunyonya) maziwa hukuta jozi ya matiti ya mama yake matamu mno
yaliyohifadhiwa yakining'inia tayari kwa kumpatia lishe kwa ajili yake. Hupata
lishe yake kutoka maziwa katika njia hii mpaka wakati huo, kwa vile mwili wake
bado ni mororo, viungo vyake na matumbo yake ni laini na dhaifu.
Bila shaka Mwenyezi
Mungu aliyeandaa utaratibu huu wa uumbaji anastahili kushukuriwa na kuabudiwa.
Jazaka Llah..kheyr.
ReplyDeleteni yeye tu الله wa kushukuriwa.
~maelezo hayo ni kutuinesha UWEZO wake kwamba yeye ni Muumbaji.....kwa hivyo tufaham kwamba hana wala hataki msaidizi ktk Uungu wake.
kujuwa hivo tujijuwe kwamba ss ni watumwa wake tu