MATENDO
YALIYO FARADHI KWA MUISLAMU
{1} Kufanya amali njema kwa moyo wa bidii na unyoofu:
Mtukufu Mtume amesema: 'Kwa hakika amali zote zinategemea nia
zake."
{2}Kumtegemea Mwenyezi Mungu:
Mwenyezi Mungu amesema:- "Na anayemtegemea Mwenyezi Mungu
yeye humtoshea"........... {Qur'an 65:3.
"Na tegemeeni kwa Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni wenye
kuamini", {Qur'an 5:23}.
{3} Kutendeana
Haki: {Kuto kudhulumiana}
Mtukufu
Mtume {s.a.w.w.} amesema:- "Haikamiliki imani ya kiumbe hadi awe na sifa
tatu, kutoa msaada wakati wa dhiki, usawa na unyoofu kati yake na mwenziwe,
mwingi wa kutoa salamu."
{4} Kuwatendea mema wazee wawili:
Mwenyezi
Mungu amesema: "Na Mola wako amehukumu kuwa msimwabudu yeyote ila yeye tu,
na kuwafanyia wema wazazi wawili. Kama mmoja wao akifikia uzee mbele yako au
wote wawili, basi usiwaambie hata Ah; Wala usiwakemee. na useme nao kwa msemo
wa heshima kabisa. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa huruma, na useme
'Mola wangu! Warehemu {Wazee wangu} kwani walinilea katika utoto".
(5} Kuwaangalia jamaa wa damu:
Mwenyezi
Mungu amesema: "Mcheni Mwenyezi mungu ambaye kwaye mnaomba na {kuangalia} jamaa
wa damu, hakika Mwenyezi Mungu ni mlinzi juu yenu". {Qur'an 4:2}.
[6) Kusaidiana mambo mema:
Mwenyezi
Mungu katika Qur'an amesema: "Saidianeni katika wema na kumcha Mwenyezi
Mungu, wala msisaidiane katika dhambi na maasi." {5:2}.
(7}Kupatanisha watu:
Mwenyezi
Mimgu amesema: "Basi mwogopeni Mwenyezi Mungu na suluhisheni mambo baina
yenu, na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ikiwa nyinyi ni katika wanao amini
{kweli}".{Qur’an 8:1}.
"Kwa hakika Waislamu wote ni ndugu, basi patanisheni baina ya
ndugu zenu. Na mcheni Mwenyezi Mungu, {msipuuze jambo la kupatanisha} ili
mrehemiwe" {Quran 49:10}.
{8}Ukweli:
Mwenyezi Mungu amesema:- "Kwa yakini Mwenyezi Mungu
atawatambulisha wale walio wa kweli na walio waongo." {29:3}.
"Mwenyezi Mungu ametuamrisha tuwe wakweli" {Qur'an 9:119}.
No comments:
Post a Comment