JINSI USHIA (UISLAMU SAHIHI)
ULIVYOIMARIKA IRAN
Katika mwaka wa 694 A.H. Falme
ya Iran ilikuwa ikitawaliwa na Ghazan Khan Mughal (ambaye jina lake la Kiislamu
lilikuwa Mahmud). Tokea wakati huo, Imani juu ya Ahlul Bait wa Mtume (s.aw.w.) iliendelea
kukua miongoni mwa wairan, kiasi kwamba Ushia ulikua kwa uimara kabisa.
Baada ya kifo cha Ghazan Khan
Muqhal mnamo mwaka wa 707 A.H., ndugu yake, Muhammad Shah Khuda Bandeh akawa
mtawala wa Iran. Aliandaa mjadala wa kidini (Mdahalo) kati ya Alama Hilli,
Mwanachuo msomi wa Kishia, na Khwaja Nidhamu’d-Din
Abdul’l-Maliki Maraghe’i, Kadhi Mkuu wa (Madhehebu) Shafii na Mwanachuo mkubwa
wa Kisunni wa wakati huo.
Midahalo Kati Ya Allama Hilli Na
Kadhi Mkuu Kuhusu Uimamu.
Nukta ya mdahalo huu ilikuwa ni
Uimamu. Allama Hilli alitoa hoja zenye nguvu sana kuthibitisha kwamba Ali
alikuwa ndiye mrithi alitemfuatia mara moja Mtume (s.a.w.w.) bila mwanya, na
kwa kuridhisha kabisa akabainisha uwongo wa madai ya ule upande mwingine, kiasi
kwamba wale wote waliohudhuria walitosheka kabisa na jinsi ya ukweli wa Allama.
Khwaja Nidhamu’d-Din alikubali
kwamba hoja za Allama haziwezi kukanushwa. Lakini akasema kwamba, kwa vile
alikuwa akifuata njia za wakubwa wake waliomtangulia, haikuwa vizuri kuiacha.
Aliona kwamba ilikuwa ni muhimu kudumisha mshikamano miongoni mwa Waislamu.
Mfalme Wa Irani Aliikubali Iman
Ya Kishi’a.
Mfalme alisikiliza hoja hizo kwa
usikivu makini, mwenyewe akaukubali msimamo wa Shi’a, na akatangaza uhalali wa
Ushia katika Iran. Hatimaye alitangaza kwa magavana wa mikoa kwamba Khutuba za
kila Ijumaa (zinazotolewa misikitini) zinapaswa zitangaze haki ya Ali kama
mrithi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).
Vile vile aliamuru kwamba
Kalimah iandikwe kwenye dinari (Sarafu za dhahabu) katika njia hii: “La ilaha
illa llah Muhammad Rasulullah, Aliyan Waliyyullah,” maana yake, “Hakuna Mungu
ila Allah; Muhammad ni Mtume wa Allah na Ali ni Walii wa Allah.” (makamu au
mlezi wa watu aliyeteuliwa kiungu). Katika njia hii mizizi ya Ushi’a ilisimama
kwa umadhubuti kabisa.
Karne saba baadaye, wakati
wafalme wa Ki-Safavid walipoingia madarakani, utando wa ujinga na ushabiki usio
na maana katika dini viliendelea kuondolewa, Ushi’a ukashamiri kila mahali
katika nchi ya Iran.
Japokuwa, wako Mazoroasti katika
Iran na dini nyingine kama Bahai. Lakini haipasi kuwahusisha na watu wa kawaida
wa Iran, ambao wana imani katika Allah na Mtume Muhammad kama Mtume wa mwisho.
Hawa wanamfuata Ali na watoto wake kumi na moja kama ilivyoamrishwa na Mtume
(s.a.w.w.).
No comments:
Post a Comment