Thursday 17 September 2015

AHLULBAYT WAMETAKASWA – HAWAFANYI DHAMBI

AHLULBAYT WAMETAKASWA – HAWAFANYI DHAMBI
Ninataka kuongelea tukio la "KlSAA" Iliposhuka Ayatut Tat'hir:- Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba (ya Mtume) na (anataka) kukutakaseni sana sana" 33:33.

Iliposhuka Aya hii Mtume alimchukua Ali na Fatima na Hasan na Husein, akawafunika nguo kisha akasema: "Ee Mola! Hawa ni watu wa nyumba yangu, basi waondolee uchafu na uwatakase sana sana." Mama Ummu Salma (mke wa Mtume) alipotaka kuingia humo, Mtume (s.a.w.) akamzuia:
Kama ambavyo kwenye tukio la Mubahala ulipofika wakati wa kuomba maombi maalum kwa ajili ya maapizano kati yake na Wakristo wa Najrani, Mtume alimchukua Ali na Fatima na Hasan na Husein tu. Ingawa wakati huo Mtume (s.a.w.) alikuwa nao wakeze, na Masahaba ambao ni marafiki zake pia, lakini hapa hawakuingia.
Wake za Mtume na Masahaba hawakuingia katika "KISAA" na hawakusimama katika uwanja wa Mubahala, kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwahusisha darja hii Ahlul Bait tu peke yao.

TAZAMA:
Tafsirul Khazin Juzu ya 3 Ukurasa wa 259
Tafsirul Ibn Kathir Juzu ya 3 Ukurasa wa 494
Tafsirul Qurtubi Juzu ya 14 Ukurasa wa 183
Zadul Masir Juzu ya 6 Ukurasa wa 381

No comments:

Post a Comment