WAUMINI WATATU WA KWANZA KATIKA UISLAMU
Katika kitabu cha Tafsir Durr-e-Manthur na katika Fathul
Qadeer cha Abu Ali Muhammad Ibn Ali al-Shawkani imeandikwa hivi kwa ushahidi wa aya ya Qurani, “Wassabiquunas
Saabiquun” (Sura 56, Aya 10-12). Ibn Abi Hatim ametoa hadithi alionena Abdullah
Ibn Abbas kwamba watakatifu WATATU ndio walioikubali (walioamini) mwanzo dini ya Kiislamu, JOSHUA mtoto wa Nun
alikuwa wa kwanza kumwamini Mtume MUSA
na mwenye imani alioamini mwanzo katika Al-Yaseen kuukubali utume wa Mtume Isa
(Tazama Sura 36, Aya 20-26) na wa tatu
wao ni Ali mtoto wa Abu Talib
aliotangulia kukubali Utume wa Mtume wetu mtukufu.
Ibn Mardwaih katika maelezo yake kuhusu Aya hiyo hiyo
ametoa hadithi kutokana na Ibn Abbas
akisema hivi kwamba aya hii yaonyesha
sifa juu ya Hizqil mwenye kuamini kati ya watu wa Firauni (Tazama Sura 40, Aya
28-33), Bwana Habib al-Najjar mwenye imani katika kabila ya Yaseen na Ali Ibn
Abi Talib, kila mmoja katika wao ni wa mwanzo kuamini kati ya watu wao, na Ali
ni bora wao kuliko wote.
Waumini hao watatu ndio waliowaongoza waislamu wakati
mitume wao walipoondoka au kufariki. Kwa hiyo habari hii inaendelea
kuthibitisha kuwa uongozi au ukhalifa baada ya Mtume ulistahili kukamatwa na
Imam Ally (a.s).
No comments:
Post a Comment