NAFASI YA AHLULBAYT KATIKA KUULINDA UISLAMU
Assalaam alaykum;
‘Tawhid’ ni miongoni mwa mambo yaliyozua mjadala mkali sana
miongoni mwa wanachuoni wa Kiislamu, wengine wakimhusisha Mwenyezi Mungu na
viungo na makazi na wengine wakiwa wanaikataa dhana hiyo, kila upande ukitoa
hoja na dalili zake. upande mmoja ni wa wanachuoni wa Madhehebu ya Sunni ambao
wanaunga mkono dhana hii, na upande mwingine ni wa wanachuoni wa Kishia ambao
wanapinga dhana hiyo.
Kunako majaliwa ya Allah (s.w) tutalishughulikia suala
hili kwa kulinganisha hoja za pande zote mbili kwa kutumia vitabu vyao vya
tawhid na vya hadith, na tutahitimisha kwa kuonesha pasina shaka yoyote kwamba
Mwenyezi Mungu yu mbali na hayo wanayo mhusisha nayo.
Sisi tunamuachia msomaji asome kwa makini na utulivu, na
uwamuzi utakuwa ni wake; bali matumaini yetu ni kwamba ataelekea kule kwenye
haki, bila ya kujali haki hiyo iko kwa nani.
Mimi kama mshia lazima niweke wazi msimamo wangu katika
kadhia hii ya tawhiid. Sisi hatuamini kuwa Allah anaonekana, wala kuwa na
viungo na hata kuhitaji makazi na pia hasafiri toka mbingu moja kwenda nyingine
kama wanavyodai mawahhabi.
Asalaam aleykum
ReplyDeletewewe unaonesha Unaelemeya saaana katika vitabu...na Qurani umeiwacha....lefe aya utufahamishe maamrisho yake...juwa siju ya hisabu kitabu Quran itakuwa Hoja kwa kila nmoja wetu..