Wednesday 11 June 2014

Dondoo Kutoka Katika Maisha Yangu ya Uislamu

Siku moja nilimtembelea binamu yangu aitwaye Abdul Muni’m. Na kabla ya kuzama jua, nilimuona katika ukumbi wa nyumba akijadiliana na mtu mmoja miongoni mwa Ikh’wanul’muslimina ambaye alikuwa mgeni nyumbani, nilisikiliza ili nione wanachojadiliana, niliharakia kuwaendea, hivyo nilipojua hali ya mjadala kuwa ni katika mambo ya dini. Niliketi karibu yao nikiangalia maendeleo ya mazungumzo ambayo Abdul’mun’im alitambulika kwa utulivu kabisa licha ya kuwepo kwa ghasia na hujuma upande wa pili, sikuwa najua aina ya mjadala kiukamilifu mpaka aliposema ndugu mwislamu: “Shia ni makafiri mazandiki!!”
Hapo nilitanabahi na niliangalia kwa makini, lilizunguka akilini mwangu swali la
kushangaza: Shia ni akina nani? Na kwa nini wao wazingatiwe kuwa makafiri? Hivi Abdul Mun’im ni Shia? Na asemayo si usemi wa kawaida, je huo ndio usemi wa Shia?!.
Kwa ajili ya kuchunga insaafu kwa kweli Abdul’mun’imu alimkwamisha hasimu wake katika kila mas’ala iliyoletwa kwenye mjadala, achia mbali busara ya maneno yake na nguvu za hoja yake.
Na baada ya kumalizika mazungumzo, na kutekelezwa kwa swala ya magharibi nilijitenga na mwenzangu Abdul’mun’im, nilimuuliza kwa heshima zote: Hivi wewe ni Shia? Shia ni akina nani? Wapi ulijuana nao?
Akasema: Polepole..... swali baada ya swali.
Nilimwambia: Samahani, mimi ningali nimeshangazwa na niliyosikia toka kwako.
Akasema: Huu ni utafiti wa muda mrefu, na ni juhudi ya miaka minne kwa taabu na
mashaka, na yasikitisha kuwa tija haijatumainiwa.
Nilimkatisha: Ni tija gani hii?
Akasema: Rundo za ujinga na kufanywa wajinga, tumeishi na hali hiyo maisha yetu yote
tukikimbia nyuma ya jamii zetu bila ya kuuliza, je dini tuliyonayo ndiyo iliyokusudiwa na
Mwenyezi Mungu (s.w.t.), nayo ndio Uislam? Na baada ya mjadala ilibainika kuwa haki
ilikuwa upande wa njia ya mbali zaidi kwa kufanya taswira kwa mtizamo wangu, nao ni
Shia.
Nilimwambia: Labda wewe umefanya haraka..... au umechanganya mambo..!
Alitabasamu huku akisema: Kwa nini wewe haufanyi utafiti kwa kuzingatia na kuvuta
subira? Na hasa ikizingatiwa kuwa ninyi mnayo maktaba hapo chuoni, itakusaidia sana kwa jambo hili. Nilisema katika hali ya (kustaajabishwa): Maktaba yetu ni ya kisunni, vipi
niutafiti Ushia?!
Akasema: Miongoni mwa dalili za ukweli wa Shia wanatoa dalili ya kuwa kwake sahihi
kutoka vitabu vya riwaya za wanavyuoni wa kisunni, humo ndio ukweli wao wadhihiri kwa sura ya wazi zaidi.
Nilisema: Hivi vyanzo vya Shia ni vilevile vyanzo vya Ahli Sunnah?!
Alijibu: Hapana, Shia wana vyanzo mahsusi vinavyovizidi mara kadhaa vyanzo vya Ahli
Sunnah, riwaya zake zote zimeelezwa na Ahlul-Bayt (a.s.) kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), lakini wao hawatolei hoja kwa Ahli Sunnah kupitia riwaya zitokazo kwenye vyanzo vyao, kwa kuwa wao masunni hawana ulazima nazo, hivyo basi hapana budi watoe hoja dhidi yao kwa dalili wanazozikubali, yaani (kulingana na usemi mashuhuri):
Walazimisheni kwa ambalo wamejilazimisha nalo wao wenyewe.
Yalinifurahisha maneno yake na mwitikio wangu kuuelekea mjadala ulizidi. Nilimwambia:
Nitaanzaje? Akauliza je katika maktaba yenu kuna Sahih Bukhari na Sahih Muslim, Musnad Ahmad, Tirmidhiy na Nasaiy? Nilisema: Ndio, tuna kiwango kikubwa cha vyanzo vya Hadith.
Akasema: Anza na hivi, kisha baada ya hapo njoo kwenye tafsiri, na vitabu vya historia, kwa kuwa katika vitabu hivi kuna Hadithi zinazojulisha wajibu wa kuifuata madrasa ya Ahlul-Bayt. Alianza kuniorodheshea mifano, pamoja na kutaja chanzo na namba ya jalada na ukurasa.
Nilisimama nimeduwaa, nikizisikiliza Hadithi hizi ambazo sijapata kuzisikia hapo kabla,

ilinifanya niingie shaka kuwepo kwake katika vitabu vya kisunni, lakini haraka sana aliikata shaka hii kwa kauli yake: Zisajili Hadithi hizi, kisha zitafute katika maktaba na tukutane siku ya Alhamisi ijayo kwa idhini yake Allah.

No comments:

Post a Comment