Friday 13 June 2014

MTUME MOHAMMAD (S.A.W.W) APEWA UANACHAMA WA SHIRIKISHO LA VIJANA WAADILIFU.

Baada ya kuwa kijana, Muhammad aliingizwa kama mwanachama wa lile Shirikisho la Wenye Maadili. Kama ilivyotajwa mapema, hili Shirikisho limejiapia lenyewe kuwalinda wayonge, kuwapinga madhalimu na waonevu, kukomesha unyonyaji wa namna yoyote ile.
Ikumbukwe kwamba ulikuwa ni ukoo wa Bani Hashim, ambao Muhammad nabii wa baadae alitokana nao, ambao ndio ulioanzisha lile Shirikisho la Wenye Maadili. Taratibu zao za kisiasa, Bani Hashim walikwishatangaza vita juu ya udhalimu na dhulma. Waliweka wazi kwamba hawatakula njama na wenye nguvu dhidi ya wanyonge; wala hawangeridhia katika unyonyaji wa maskini kwa Maquraishi wa Makka.
Sio miaka mingi baadae, Muhammad alikuwa aanzishe utaratibu wa ujenzi upya wa jamii ya wanadamu, sehemu ya uchumi ambayo itatambua wazi uharibifu wa unyonyaji. Angezichukua zile "fursa" za Maquraishi na "haki " zao za kunyonya maskini na wanyonge, kutoka kwao.
"Lile Shirikisho la Wenye Maadili linaelekea kuchukua sehemu muhimu sana katika maisha ya Makka, na kwa sehemu kubwa kuelekezwa kwa watu na sera ambazo baadae Muhammad alijikuta anapingana nazo. Hususan ukoo wake wa Bani Hashim ulikuja kuwa na wajibu mkubwa katika Shirikisho la Wenye Maadili."

(Muhammad, Prophet and Statesman, 1961)

No comments:

Post a Comment