Friday 13 June 2014

Kueneza chuki dhidi ya Ushia na dhidi ya Iran ndiyo silaha ya mabeberu

Siku ya Jumanne ilikuwa ni siku ya kuadhimisha sikukuu ya mab'ath ya kupewa Utume Mtume wetu Muhammad SAW.  Sambamba na maadhimisho ya sikukuu hiyo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi ameonana na maafisa wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, matabaka mbali mbali ya wananchi na wageni wanaoshiriki kwenye mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu pamoja na mabalozi wa nchi za Kiislamu waliopo nchini Iran.
Huku akisisitizia udharura wa ulimwengu wa Kiislamu kulipa umuhimu mkubwa suala la kutafakari mambo kwa kina, kuwa na muono mpana na wa mbali, kuwa na fikra zinazojenga na kuwa na welewa wa kutosha na wa kweli kuhusiana na kambi ya maadui wa umma wa Kiislamu na vile vile kushikamana umma wa Kiislamu na kutozipa nguvu tofauti za kiitikadi na utaifa amesisitiza kuwa, leo hii bendera ya Uislamu imeshapeperushwa juu, na moyo wa kujitambulisha Kiislamu Waislamu duniani umepata nguvu sana sasa hivi ikilinganishwa na huko nyuma.
Amesema, taifa la Iran pia kutokana na kuwa na dhana nzuri na kuwa na imani na msaada wa Mwenyezi Mungu, limo katika kupiga hatua za kimaendeleo na kuyaweka nyuma matatizo sambamba na kupata ushindi mtawalia katika mapambano yake na dhulma, ujahili na ukosefu wa uadilifu.
Ayatullah Udhma Khamenei, aidha ametoa mkono wa baraka kwa mnasaba wa maadhimisho ya siku ya kubaathiwa na kupewa Utume, Mtume wa Uislamu SAW na kusema kuwa, sababu kubwa ya kutumwa Mitume wa Mwenyezi Mungu hususan Mtume wa Uislamu SAW ni kuwaongoza watu kwenye kutumia akili, hekima na kutafakari mambo kwa kina.
Ameongeza kuwa: Iwapo suala la kutafakari kwa kina mambo na kutumia nguvu ya akili na muono wa mbali litaenea katika jamii ya Waislamu, basi bila ya shaka yoyote matatizo mengi ya ulimwengu wa Kiislamu yatatatuka.
Vile vile ameashiria namna baadhi ya watu wanavyoyafahamu kimakosa mafundisho ya Uislamu na Qur'ani Tukufu na jinsi wasivyo na elimu ya kutosha kuhusu mafundisho hayo matukufu na kusema: Kutokuwa na mtazamo sahihi na kushindwa kuwa na welewa wa kina kuhusiana na mafundisho matukufu ya Uislamu na Qur'ani Tukufu kumepelekea leo hii baadhi ya watu watumie jina la Uislamu kuwadhulumu Waislamu wengine na hata kuwaua kwa umati ambapo hali ni mbaya kiasi kwamba imefikia hadi huko barani Afrika watoto wa kike wasio na hatia wanatekwa nyara kwa kutumia jina la Uislamu.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aidha ameashiria mfano mwingine ambao ndani yake nguvu ya akili na kutafakari mambo kwa kina inabidi itumike vizuri katika mazingira ya hivi sasa ya ulimwengu wa Kiislamu na kusema kuwa: Leo hii maadui wametangaza vita vya wazi dhidi ya Uislamu na silaha kubwa inayotumiwa na maadui hao ni kuzusha mizozo na hitilafu za kiitikadi na vita baina Waislamu wa Kishia na Kisuni na kama kama nguvu ya akili na kutafakari kwa kina mambo itatumizuri ika vbasi itawezekana kuuona mkono wa adui na shabaha zake na kutotumbukia kwenye njia ya kufanikisha malengo ya watu wanaoitakia mabaya dini tukufu ya Kiislamu.
Ayatullah Udhma Khamenei, ameutaja mshikamano na kuundwa umma mmoja wa Kiislamu kuwa ni miongoni mwa mahitaji ya dharura kwa ulimwengu wa Kiislamu na huku akisisitiza kuwa moja ya shabaha kuu za kuzusha mirafakano kati ya Waislamu na kueneza chuki dhidi ya madhehebu ya Kishia na dhidi ya Iran, ni kambi ya kibeberu kutaka kuficha matatizo yake na kuulinda utawala ghasibu wa Kizayuni.
Ameongeza kuwa: Kinachotarajiwa kutoka kwa mataifa ya Waislamu hususan wasomi, wanafikra na watu wenye vipaji na ushawishi katika ulimwengu wa Kiislamu ni kuwa na tadibiri na mtazamo mpana na wa mbali na kuitambua vilivyo kambi ya maadui wa umma wa Kiislamu na kwa njia hiyo ndipo itawezekana kutambua vizuri uhakika huo ulio wazi.
Vile vile amesisitiza kuwa, duru za kisiasa za Magharibi hivi sasa zinaeneza ujahilia ule ule ambao Bwana Mtume Muhammad SAW alitumwa na Mwenyezi Mungu kuja kupambana nao na kuuangamiza. Amesema: Ukosefu wa uadilifu, ubaguzi, kutojali heshima ya mwanadamu, kuyachanganya pamoja masuala ya kijinsia na kupiga propaganda za kuchochea uchafu wa kimaadili na wanawake kutembea uchi, yote hiyo ni mifano ya utamaduni fasidi wa Kimagharibi ambao kwa hakika ni kurejea kwenye ujahilia ule ule wa zama za huko nyuma ingawa kwa sura mpya ya kisasa.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia njama kubwa zinazofanywa na maadui kwa lengo la kuzima mwamko wa Kiislamu na kusema kuwa: Ingawa njama hizo za maadui zinaonekana kijuu juu kuwa zimefanikiwa katika baadhi ya maeneo, lakini uhakika wa mambo ni kuwa, haiyumkiniki na ni muhali kukandamiza na kuzima mwamko wa Kiislamu.
Ayatullah Udhma Khamenei amegusia pia hatua za maendeleo zilizopigwa na taifa la Iran chini ya kivuli cha kuwa na imani na ujumbe aliokuja nao Bwana Mtume Muhammad SAW na mshikamano wa ndani wa taifa hili na ushujaa wake katika kukabiliana na adui pamoja na kuwa na hisia za matumaini kutokana na ahadi za nusra na msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu akiongeza kuwa: Leo hii kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu, serikali yenye nguvu mpya ya Iran na watendaji wake wanafanya kazi kubwa katika medani tofauti wakiwa na hisia za kulinda heshima ya Uislamu.
Kiongozi Muadhamui amekutaja kuweko matatizo na changamoto mbali mbali katika maisha ya mwanadamu kuwa ni jambo la kawaida kabisa na kuongeza kwamba: Watu wenye hekima na tadibiri huwa wanakubali kuvumilia matatizo kwa ajili ya kufikia kwenye heshima, hadhi ya mwanadamu na kuwa karibu na Mwenyezi Mungu lakini watu wasio na hekima, badala ya kuikubali Wilaya na uongozi wa Allah, wanakimbilia kwenye utawala wa mashetani na matokeo yake ni kujidhalisha na kujidunisha mbele ya mashetani hao.
Ayatullahil Udhma Khamenei ameendelea kulitolea ufafanuzi suala hilo kwa kuzungumzia kalibu na misingi iliyowekwa na Qur'ani Tukufu akisema: Kwa mujibu wa aya za Qur'ani Tukufu, watu ambao katika kutafuta heshima wanaacha Wilaya na uongozi wa Mwenyezi Mungu na kukimbilia kwa maadui wa Uislamu na ubinadamu na kwenye utawala wa mashetani, hatima yao ni kuwa duni na kamwe hawawezi kupata heshima bali hawatapata shukrani hata kutoka kwa hao mashetani wanaojidhalilisha kwao.
Amesisitiza kuwa: Tunapaswa kujifunza kutokana na fomula na msingi huu uliobainishwa na Qur'ani Tukufu na kuitambua njia sahihi na ya kweli ya kutufikisha kwenye ufanisi wa kweli ambayo ndiyo hiyo njia ya uongofu wa Qur'ani Takatifu.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameitaja siri ya mafanikio na ushindi wa kila namna wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nyakati tofauti kwenye mapambano mbali mbali ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kimataifa kwamba ni kutegemea na kuwa na nia nzuri na ahadi za Mwenyezi Mungu na kusisitiza kwamba: Hiyo ndiyo njia ya taifa la Iran na katika siku za usoni pia njia ya taifa hili itakuwa ni hiyo hiyo.
Mwishoni mwa hotuba yake, Ayatullah Khamenei amemuomba Mweyezi Mungu ammiminie rehema Zake Imam mtukufu (Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu) kutokana na kutufungulia njia hii. Vile vile amemuomba Allah awamiminie rehema Zake mashahidi waliomwaga damu zao katika njia hii na rehema za Mwenyezi Mungu zilishukie taifa la Iran ambalo limethibitisha uimara wake katika hatua na vipindi vyote vya njia hii na rehema za Allah ziwafikie pia viongozi na maafisa wote wanaohusika katika ufanikishaji wa njia hii na ambao wako tayari wakati wote kujitolea na kufanya jitihada kubwa katika njia hiyo.
Kabla ya miongozo hiyo ya Kiongozi Muadhamu, Hujjatul Islam Walmuslimin Hassan Rouhani, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mkono wa baraka kwa mnasaba wa maadhimisho ya siku ya kupewa Utume Mtume Muhammad SAW na kusema kuwa, mab'ath ni ufufuo mkubwa katika historia na ni neema kwa ajili ya kutumia vizuri akili kulingana na wahyi utokao kwa Mwenyezi Mungu.
Amesema, Bwana Mtume Muhammad SAW aliweza kuzivutia nyoyo kwa upole na maadili yake adhimu na kumtunukia mwanadamu elimu, uhuru na umaanawi.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameitaja mifarakano, ukosefu wa uadilifu, machafuko na misimamo mikali ya kufurutu ada kuwa ni matatizo makubwa ambayo kambi ya ukafiri imeutwisha ulimwengu wa Kiislamu na kuongeza kuwa: Leo hii Mapinduzi ya Kiislamu yanalingania umoja, mshikamano na kuwekwa pembeni hitilafu ndogo ndogo katika umma wa Kiislamu ili umma huo uweze kusimama kwa nguvu moja kupambana na kambi ya kufru.


No comments:

Post a Comment