Wakati Muhammad alipokuwa na umri wa miaka ishirini, ilizuka vita
miongoni mwa Maquraish, kabila lake, na kabila la Hawazin. Ingawa alikuwapo
katika kampeni za vita hii, hakushiriki kwenye nafasi yoyote katika mapigano.
Hakuua au kujeruhi mtu yoyote, hivyo kuonyesha katika kipindi hiki cha mwanzo
cha maisha yake, kuchukia kwake umwagaji wa damu. Anasemekana, hata hivyo,
kuwahi kuokota mishale kutoka uwanjani, na kuitoa kwa ami zake ambao walikuwa
wanapigana.
Huu ndio msimamo wa Mtume mpaka alipokufa hakuwahi kuivamia nchi
yoyote. Kazi ya Mtume ilikuwa kuwalinda waislamu dhidi ya mashambulizi na wala
sio kuanzisha mashambulizi kama wafanyavyo leo baadhi ya watu wanaodai kuwa ni
waislamu. Kila palipotokea mwanya wa kufanya mazungumzo ya amani alifanya hivyo
mara moja ili kuepusha vita. Angalia vita ya Khandaq imefanyikia katika mji wa
Madina, yaani makafiri walisafiri mamia ya maili kwenda kuwashambulia waislamu,
hapo hakuna njia nyingine isipokuwa kuhihami. Vita ya Uhudi nayo imefanyikia
kwenye eneo la Uhudi ambalo ni jirani na Madina, hata vita ya Badri ilifanyikia
karibu na Madina.
No comments:
Post a Comment