Friday 13 June 2014

FIKRA ZA KIWAHHABI NI KUYAKUFURISHA MADH-HEB NA KUPANDA MBEGU YA CHUKI NA UTENGANO MIONGONI MWA WAISLAMU.

Enyi Waislam wenye utambuzi,
Asalaam alaykum. Mmesoma nasiha za mara kwa mara kutoka mtandao wa alhidaaya.com. Huu ni mtandao wa Mawahhabi ambao lengo lao ni kuwapotosha Waislam, kuleta chuki na utengano miongoni mwa Waislam na kuwakufurisha wote ambao sio Mawahhabi. Watu hawa ni muhimu sana wawaambie Waislam asili ya dini yao, wametoka wapi, walipotea wapi na wafanye juhudi gani sasa ili wote tushikamane na kamba ya Mwenyezi Mungu na wala tusifarakiane. Na wanaogopa kurudi kwenye tarekh maana tarekh itawaumbua. Ni bahati mbaya sana kwamba wamenasa ktk fikra potofu za kiwahhabi na kuwa wafuasi wa Muawiyyah na Yazid na inshallah Mwenyezi Mungu ni Mlipaji Bora kabisa.
Naam maneno yangu haya yana ushahidi. Nitamchukia na kumpinga sana yeyote, kwa ushahidi madhubuti sio ushahidi blaa blaa na ninapofanya hivyo sijali yeyote mradi tu nautetea Uislam Mtukufu, Mtukufu Mtume(s.a.w.w) na Ahlul Bayt Rasulullah(s.a.w.w) na ikiwa kufanya haya ni kuwa rawafidha basi mimi ni rawafidha mkubwa.
Ewe msomaji mtukufu,
Kipo kitabu kiitwacho "AS-HIATU-WA AT-TASHAYUU" kilichotungwa na Mpakistani mwenye chuki ambaye ni miongoni mwa wanaofadhiliwa na Mawahhabi, jina lake ni Ihsan Ilahi Dhahir na kimechapwa Saudia. Na ndani yake mtungaji anazitupa tuhuma na uzushi dhidi ya Ushia, na anadai kwamba yeye anaeleza kutokana na vitabu na rejea za Mashia.
Kwa mfano, utaona katika uk wa 20 wa kitabu hicho, anataja neno la Al-Marhum Al-Ustadh Mheshimiwa Sheikh Muhammad Hussein Al Mudhafar, kisha analisherehesha kufuatana na vile apendavyo yeye na vile nafsi yake inayoamrisha maovu inavyomtuma.
Tunaweka wazi neno hilo pamoja na sherhe ya Wahhabi huyu ili uone mwenyewe jinsi Mawahhabi waliofilisika kwa dalili, wanavyotegemea maneno ya tuhuma, uzushi na uongo dhidi ya Shia. Mar-hum Al-Mudhafar anasema:
"Fakanatid-Daawatu Littashayui Liabil-Hassan Alayhis-Salaam Min Sahihir-Risalat Salallahu Alayhi Waalihi Wasallam Tamshi Minhu Janban Liyanbi Maad-dawat Lish-Shahadatayn"
Tafsir Yake:
Mwito kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kumfuata Abul Hassan Ali(a.s) ulikua ukienda sambamba na mwito wa Shahada mbili.
Na maana ya maneno yake haya ni kwamba:
Ushia haukuzalikana kutokana na hali ya kimazingira wala sio madhheb yaliyoanzishwa baadaye, bali ni Madh-heb ya asili ambayo chanzo chake kinaanzia kwa mwenyewe Mtume Muhammad (s.a.w.w), kwani Mtume (s.a.w.w) alikua akilingania watu juu ya Uimam wa Amirul-Muuminina Ali(a.s) sambamba na wito wa Shahada mbili.
Kisha Wahabi huyu muovu anayawekea Taaliq maneno ya Sheikh Mudhafar na anasema:
"Hakika Mtume (s.a.w.w)[kwa mujibu wa madai ya Mudhafar] alikua akimfanya Ali kua ni mshirika wake katika Unabii wake na ujumbe wake"!!!
iwapo mwandishi huyu sio mtumwa wa matamanio yake yenye chuki na mwenye kufadhiliwa na Mawahabi, na iwapo ni mchunguzi wa Itikadi za Kiislam za Kishia angesema na kusimamia Haki.
Uk 49 anatuhumu Ushia kwamba umepokea fikra zake kutoka kwa Abdallah Bin Sabaa aliyezalikana kutoka kwa Myahudi wa Yemen, na anavyoitakidi Tabari ni kwamba Abdallah Bin Sabaa alidhihirisha Uislam na kuficha Uyahudi na mapenzi yake kwa Imam Ali(a.s) aliyafanya kifuniko cha kueneza fikra zake.
Mwandishi huyu wa Kiwahhabi anategemea mambo aliyoyapokea Tabari kuhusu uzushi huu, Amma sanad ya riwaya ambayo Tabari anaielezea ni kama ifuatavyo neno kwa neno:
"Aliniandikia As-Sariyyu kutoka kwa Shuaib, kutoka kwa Seif, kutoka Atiyyah naye toka kwaYazid Al-Faq-Asi: Abdallan Bin Sabaa alikuwa Myahudi katika watu wa Sanaa...."[vile vile ameipokea riwaya hii Ibn Khaldun Al-Magharib na Ibn Kathir Ash-Shami na walio mfano wa Tabar miongoni mwa maadui wa Ahlul-Bait].
Sasa tunaiweka riwaya hii kwenye meza ya uchunguzi.
Kwa mtazamo wa haraka ndani ya vitabu vya elimu ya rijali (ambavyo vimeandikwa na wanachuoni wa Kisunni) vitatutosheleza kufahamu hali za wapokezi hawa:
1)As-Sari sawa sawa akiwa ni As-Sari Ibn Ismail Al-Kufi au As-Sari Ibn A'sim aliyekufa mwaka 258 kila mmoja wao ni miongoni mwa waongo na wazushi.
Tazama:
a)Tahdhibut-Tahdhib cha Ibn Hajar Juz 3 uk 46
b)Tarekh Al-Khatib Juz 1 uk 193
c)Mizanul-Itidal Juz 1 uk 37
d)Lisanul Mizan Juz 3 uk 13
2)Shuaib Ibn Ibrahim A-Kufi: Majhul
[Hatambulikani hali yake] Tazama:

a)Mizanul-Itidal Juz1 uk 447
b)Lisanul-Mizan Juz 3 uk 145.
Haya ndiyo mategemeo ya uzushi na uongo wa Mawahhabi dhidi ya Ushia. Hawa ndio watetezi wa Tawhid na Sunna. Wao ni wapenzi na watetezi wa Muawiya na Yazid wauaji wa Bwana wa Vijana wa Peponi Imam Hussein(A.S) na watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w)Na malipo mema yapo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

No comments:

Post a Comment