Hitilafu baina ya Shia na Waislamu wengine wasio Shia haikuanza
juzi na jana. llianza karne nyingi zilizopita; mara tu baada ya Mtume Muhammad
s.a.w.w. kufariki dunia. Hata hivyo, katika kipindi cha Makhalifa wawili wa
kwanza, hitilafu hiyo haikuzusha zogo na fitina kubwa kama lile lililozuka
katika kipindi cha Makhalifa wa tatu na wa nne.
Baada ya Khalifa wa tatu (Khalifa Uthman) kuuliwa, na mtu
aliyekiitwa Muawiya kuongoza upinzani dhidi ya Khalifa wa nne (Imam Ali), ndipo
hitilafu hiyo ilipopaliliwa moto. Na kutokana na upinzani huo ndipo Imam Ali
a.s. alipolaaniwa, kwa amri ya Muawiya, katika hotuba zote za Ijumaa, kwa muda
usiopungua miaka themanini. Ndipo wote wale waliokimtambua Imam Ali a.s. kuwa
ni imamu wa haki (yaani Shia) walipokuwa wakisakwa kama nyoka na kuuawa! Ndipo
Imam Hassan a.s., mjukuu wa Mtume s.a.w.w., alipouliwa kwa kutiliwa sumu
chakulani mwake! Ndipo Imam Hussein a.s., mjukuu mwingine wa Mtume s.a.w.w.,
alipouliwa kinyama huko Karbalaa (lraq) kwa kukatwa kichwa chake, Kikatungikwa
kwenye mkuki na kuchezewa ngoma, na kuliacha pingiti la mwili wake
lishetwe-shetwe na farasi! Ndipo hofu ilipofikia kiwango cha watu, chini ya
Ufalme wa Muawiya, kuogopa kuwapa watoto walio wazaa jina la Ali! Ndipo hata
mashekhe, kwa kuchelea kuadhibiwa na kuuawa, walipokiogopa kulitaja jina la
Imam Ali a.s. katika riwaya za Hadith za Mtume s.a.w.w.; badala yake ikawa
husema: 'Amesema Sheikh'!
No comments:
Post a Comment