Imekuja na kuelezwa katika maana ya
neno Shaaban kauli nyingi sana. Na kati ya kauli hizo ni yale yaliyo semwa
na Ibnu mandhuur katika lisaanul-Arab juzu ya kwanza: (Kwa hakika umeitwa kwa
jina la Shaaban kwa sababu umedhihiri na kuwa kati ya mwezi wa Ramadhani na
Rajabu, na wingi wake ni Shaabaanaati, na Shaabaini, na Shaaban: Ni kizazi
kitokanacho na Hamdan, Kilitoka katika vizazi vya Yemen, Na kwenye kizazi hiki
hunasibishwa Aamir As-sha’abiy, na imesemekana: Shaaba ni jabali lililoko
kwenye nchi ya Yemen, nalo ni lenye mapango au mabonde mawili).
Na muandishi wa Al-munjid fi llugha
amesema: (umeitwa kwa jina hilo kutokana na waarabu kutawanyika na kusambaa
ndani ya mwezi huo katika kutafuta maji).
Ama yaliyo kuja kutoka kwa Mtume wa
Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) ni kauli yake isemayo: (Kwa hakika umeitwa kwa jina la
Shaaban kwa sababu ndani ya mwezi huo hutawanyika riziki za waumini).
Na amesema (s.a.w.w)
(Kwa hakika umeitwa kwa jina la Shaaban kwa sababu hudhihiri ndani yake kheri nyingi
kwa ajili ya Ramadhan).
No comments:
Post a Comment