Monday 16 June 2014

IMAM MAHDI

As-salamun alaykum
Je itikadi ya uwepo wa Imam Al-Mahdi {atf} ni ya kimadhehebu tu, au ni ya kidini?
Ndugu msomaji kumekuwa na tuhuma nyingi na fikra mbalimbali kutoka kwa wale wasioyajuwa ya kidini na kuyasambaza pasi na kuwa na elimu nayo, kama zile za kuambiwa eti mashia wanaitikadi mpya ya ujio wa kiongozi wa kumi na mbili ajulikanaye kama Muhammad bin Al-hassan Al-mahady {atfs}. Lakini la kustaajabisha hapa ni kuwa, ukirejea vitabu vingi vya waisilamu na pia vikiwemo vya wasambazaji wa tuhma hizi, utakuta yapo ndani ya vitabu vyao yakitajwa kwa uwazi kabisa. Kwa hiyo dini zote zinaitakidi kuwa ni lazima kuje mtu atakaewaokoa watu kutokana na madhalimu na kuijaza ardhi uadilifu na usawa baada ya kuwa umejaa dhulma na jeuri [kama alivyosema Mtume {s.a.w}] katika zama za mwisho, ila sasa tofauti ni kuhusu mtu huyo ni nani?! Kwa upande wa Wakiristo wakasema ni Nabii Issa {as}, na kwa upande wa dini tukufu ya kiisilamu wakasema ni Mmoja kati ya watu wa nyumbani kwa Mtume {saww} ambaye ni Al-Mahdy {atfs}.
Lakini utofauti pia wa madhehebu ya kiisilamu ukawepo, kama hivi; amezaliwa au laa?! Ni Hassaniyu au Hussainiyu [yaani ni katika kizazi cha Imamu Hassan au Hussain {as}]?! Sasa ilipofikia hapa, wenzetu Ah-lusunna wal-jamaa wakasema hakuzaliwa bali atazaliwa katika zama za mwisho, naye ni katika kizazi chake Mtume {saww}. Na kwa Madh-hebu ya Ah-lulbayt{as} wao wakasema ameshaazaliwa na tena ilikuwa ni 15/Shaabani/255 H. na kuuchukuwa uimamu baada tu ya kufariki baba yake Imamu Al-skary{as} mwaka 260 H .Na kuhusu hili maulamaa wengi sana wakiah-lulsunna wameliandikia vitabu maalumu kabisa kama jedwali linavyoonyesha hapa chini:


1 Al-kan-njii Al-bayani fy Akh-baris-swahaba
2 Mulla Ally Muttaqy Al-burhan fy Alaamaat Mahady akhiru zamaan
3 Al-haafidh Suyutwy Al-urful-wardy fy Akh-bar Al-mahady
4 Ibnu Hajar Al-qaulul-mukh-taswar fy Alaamaat Al-mahadil-muntadhar
Pia kwa kumalizia Qur’an nayo ikatuelezea kuwa katika zama hizo ardhi itamilikiwa na Waja wema:“Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya kumbukumbu, kuwa ardhi watairithi waja wangu wema”. {Al-anbiya’a: 105}. Na kuhusu Bw: Mtume {saww} akasema: “Itakuwaje kwenu nyinyi-katika zama hizo- atakaposhuka Masiihu bun Mariamu {as} na Imamu wenu akiwa naye”.!! Swahihul-bukhary [kwa sherehe ya Al-karmaany] ;juz;14 uk;88.Na nyinginezo ayah nyingi na hadithi kuhusu jambo hili adhim kabisa mbele ya uisilamu tulizoziacha kwa ufipisho wa karatasi yetu.

No comments:

Post a Comment