Sunday, 15 June 2014

FADHILA ZA MATENDO YA MWEZI WA SHAABAN

Imekuja katika Tafsiri ya Imam Hasan Askariy (a.s) kuhusiana na matendo ya mwezi mtukufu wa Shaaban riwaya ifuatayo:
(Na kwa hakika Amirul-muuminiin (a.s) alipita kwa kaumu fulani kati ya waislaam waliojumuika mahala pamoja, ndani yake kukiwa hakuna Muhajiriina wala answari, nao wakiwa wameketi katika baadhi ya misikiti. Katika siku ya kwanza ya mwezi wa Shaaban, mara akawasikia wakizungumza kuhusiana na suala la usiku wa Qadri, na mambo mengine kati ya mambo waliyo tofautiana kwayo watu, na sauti zao zikiwa zimepaa juu, na ubishani na majadiliano kuwa makali kati yao, mara Mtume (a.s) akasimama na kutoa salam na wao kumpatia nafasi, na wakaanza kumuuliza kuhusu sababu ya kukaa kwake kati yao, nae akasema kuwambia na kuwaita:

 Enyi watu wenye kuzungumzia mambo yasiyo wahusu, -Enyi wazuaji wa bidaa, hii ni siku ya mwanzo ya mwezi mtukufu wa Shaaban, mola wetu ameuita kwa jina la Shaaban,  kutokana na kutawanyika na kudhihiri ndani yake kheri nyingi, hakika Mola wenu amefungua ndani ya mwezi huu milango ya pepo, na akakutandazieni na kukuonyesheni ndani yake majumba yake ya kifakhari na kheri zake zilizo nyingi ndani ya mwezi huu, na kwa thamani ndogo na kwa mambo mepesi, basi nunueni vitu hivyo, na Iblisi alie laaniwa akakutangazieni na kukuanikieni, kundi la shari zake na mabalaa yake, kwa hivyo nyinyi si vinginevyo bali nyinyi mnazidi kudidimia katika uovu na upotevu, na mnazidi kushikamana na matawi ya ibilisi, na mkijitenga na kujiweka mbali na matawi ya kheri, iliyo funguliwa milango yake kwa ajili yenu, Na huu ni mwezi mtukufu wa Shaaban na kheri zake zilizo nyingi:

Swala, Funga, Zaka, Kuamrisha mema na kukataza Mabaya, na kuwatendea wema wazazi wawili, na watu wa karibu, majirani na kusuluhisha kati ya watu walio gombana, na kutoa sadaka kwa mafukara na masikini, mnajilazimisha kufanya mambo yaliyo ondolewa kwenu, na mambo mliyo zuiliwa kuyazungumzia, kwani kufichua na kupembua siri za Mwenyezi Mungu, ambazo mwenye kuzipembua na kuzikashifu atakuwa ni miongoni mwa watu walio angamia, ama kwa hakika nyinyi lau kama mnge simama juu ya yale mliyo andaliwa na Mola wetu alie takasika, kwa ajili ya watiifu kati ya waja wake katika siku hii, basi msinge pata muda wa kujishughulisha na haya myafanyayo, na munge anza kufanya yale mliyo amrishwa kuyafanya, wakasema: Ewe amiril-muuminiin, ni mambo yapi aliyo yaandaa Mwenyezi Mungu katika siku hii kwa ajili ya waja wenye kumtii yeye? Amirul-muuminiin (a.s) Akasema:

Sinta kuhadithieni isipokuwa niliyo yasikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w)- hadi akafikia kusema-kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: Ninaapa kwa haki ya yule alie nituma kwa haki kama mtume, hakika Iblisi inapofika siku ya kwanza ya mwezi wa Shaaban, hutawanya majeshi yake katika pembe zote za ardhi na kona zake, anawambia: jitahidini kuwavutia baadhi ya waja wa Mwenyezi Mungu kwenu katika siku hii, na hakika Mwenyezi Mungu alie takasika, amewatawanya malaika katika pembe zote za ardhi na kona zake, anasema kuwambia: watieni uimara waja wangu na waongozeni, na wote watapata saada kupitia kwenu isipokuwa atakae kataa, na kupetuka na kufanya jeuri, hakika huyo atakuwa katika kikundi cha iblisi na wanajeshi wake, hakika Mwenyezi Mungu alie takasika inapofika siku ya kwanza ya mwezi wa Shaaban, huamrisha milango ya pepo ifunguliwe, na huuamrisha mti wa Tuuba uchomoze matawi yake juu ya dunia hii, kisha mnadi wa Mola wetu alie takasika huita:

 Enyi waja wa Mwenyezi Mungu, Haya hapa matawi ya mti wa Tuuba…, basi shikamaneni nayo yatakuinueni hadi peponi, na haya hapa matawi ya mti wa Zaquum basi jihadharini na matawi hayo yasikupelekeni kwenye moto wa jahiim, Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): Ninaapa kwa haki ya yule ambae amenituma kwa haki kama Mtume, hakika mwenye kuuendea mlango wa mambo ya kheri na mema katika siku hii, hakika atakuwa ameshika tawi moja wapo katika ya matawi ya mti wa Tuuba, basi litampeleka na kumfikisha peponi, na mwenye kushikilia mlango wa shari katika siku hii, basi atakuwa ameshikilia tawi moja wapo kati ya matawi ya mti wa Zaquum, nalo litampeleka hadi Motoni, kisha Mtume ( s.a.w.w) akasema:


No comments:

Post a Comment