VITABU VYA HADITH VINAVYOCHAPISHWA SIKU HIZI VINACHAKACHULIWA KUONDOA
MADAI YA MASHIA KAMA WANAVYOFANYA WAKRISTO KUONDOA ATHARI ZA UISLAMU KWENYE
BIBLIA.
mengi ya matoleo
mapya ya vitabu hivyo yamefanyiwa mabadiliko na baadhi ya sehemu kuondolewa,
hususan zile zinazounga mkono madai ya Shia. Ufuatao hapa chini ni mfano mdogo
tu wa yanayofanywa katika
vitabu hivyo:
Katika ukurasa wa
301 wa juzuu ya 3 ya Tafsir al-Kashshaaf iliyokusanywa
chini ya maelekezo ya Sheikh Mustafa al-Halabi (toleo la pili, 1319 A.H.
liliochapishwa na Main Government Printing House ya Amiriah Bulaq ya Misir),
kuna beti zinazojitokeza ambazo kwazo Jarullah Zamakhshari, mfasiri wa al-Kashshaaf, alitangaza
wazi imani yake katika
uhalali wa Ushia.
Lakini katika chapisho la 1373 A.H. lililochapishwa na Printing House Istiqamah
bi’l-Qahara, shairi lililotajwa halionekani tena.
Marehemu Allamah
Sayyid Akhtar Rizvi katika kitabu chake Uimamu uk. 37, anaandika kushangazwa kwake
kutokana na maneno yaliyoondolewa katika kitabu cha at-Tarikh cha
at-Tabari, chapa ya Leiden (ya mwaka 1879 Masihia) ambayo imeyanakili maneno ya
Mtukufu Mtume (s.a.w.) aliyoyatumia wakati wa karamu maarufu ya ndugu wa karibu
aliyoitayarisha mwenyewe.
Maneno ya mwisho
aliyoyasema Mtukufu Mtume (s.a.w.) katika karamu hiyo yalikuwa haya: “Enyi watu
wangu! Huyu Ali ni ndugu yangu, wasii wangu na khalifa wangu miongoni mwenu;
msikilizeni na mtiini.” Lakini katika chapa ya Misri (ya mwaka 1963 Masihia) - chapa
ambayo inayodaiwa kuwa imechekiwa na ile ya Leiden - maneno haya muhimu:
“wasii wangu na
khalifa wangu” yamebadilishwa na kuwa “kadha wa kadha” na kusomeka hivi: “Huyu Ali ni ndugu yangu na
kadha wa kadha.” Huu ni msiba mkubwa.
No comments:
Post a Comment