WAULIZENI WENYE KUMBUKUMBU IKIWA NINYI HAMJUI (QUR. 16:43 NA 21:7)
Bila shaka aya
hii Tukufu inawaamuru Waislamu kuwarejea watu wenye kumbukumbu kwa kila
linalowatatiza ili wapate kuufahamu muelekeo ulio sawa, kwani Mwenyezi Mungu
amewaandaa (wenye kumbukumbu) kwa ajili hiyo baada ya kuwafunza, basi wao ndiyo
waliobobea katika elimu na ndiyo wanaofahamu Ta'wili ya Qur'an.
Kwa hakika aya
hii ilishuka kuwatambulisha Ahlul-Bait (a.s.) nao ni Mtume Muhammad, Ali,
Fatma, Hasan na Husein, na hili lilitendeka katika zama za Mtume. Amma baada ya
Mtume (s.a.w.w.) mpaka kitakaposimama Qiyama (wenye kumbukumbu) ni hawa hawa
watano waliotajwa ambao ndiyo Ahlul-Kisaa na huongezwa kwa hao, Maimamu tisa
kutoka katika kizazi cha Hussein (a.s.) ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu
amewabainisha katika Minasaba mbali mbali na akawaita kuwa ni Maimamu wa
uongofu na ni taa ziondoazo kiza na wao ndiyo wenye kumbukumbu, na ndiyo
waliobobea katika elimu, Mwenyezi Mungu amewarithisha elimu ya kitabu.
Riwaya hizi
zimethibiti na ni sahihi tena mutawatir kwa Mashia tangu zama za Mtume
(s.a.w.w.), na wamezieleza baadhi ya wanachuoni wa Kisunni, na wafasiri wao
wamekiri kwamba kushuka kwa aya hii kunawahusu Ahlul-Bait (a.s.). Ninawataja
miongoni mwa wanachuoni hawa kwa kutolea mfano:
1) Im1)Imam
Thaa'labi katika Tafsiri yake (alipozunhumzia) maana ya aya hii katika Surat
An-NahliNahl.
3)
Tafsirul-Qur'an ya ibn Kathir Juzuu ya pili ukurasa 570570.
3)
Tafsirut-Tabari, Juzuu ya kurni na nne ukurasa 109.
4)
Tasirul-Alusi iitwoyo Ruhul-Maani Juzuu ya kumi na nne ukurasa wa 134.
5)
Tafsirul-Qurtubi Juzuu ya kumi na moja ukurasa 272.
6)
Tafsirul-Hakim iitwayo Shawa-Hidut-Tanzil,
Juzuu ya kwanza ukurasa 334.
7) Tafsir
At-Tustari, itwayo Ih-QaaQul-Haq, Juzuu ya tatu ukurasa 482.
8)
Yanahi'ul-Mawaddah cha Al-Qanduzi Al-Hanafi ukurasa wa 51 na 140.
Na ilivyokuwa
wenye kumbukumbu kwa dhahiri ya aya ni Ahlul-Kitab miongoni mwa Mayahudi na
Wakristo, basi imetulazimu juu yetu kubainisha wazi kwamba wao sio
waliokusudiwa katika aya hiyo Tukufu.
Kwanza; Kwa sababu Qur'an Tukufu imewataja (Mayahudi na Wakristo) mara
nyingi katika aya nyingi kwamba wao waliyageuza maneno ya Mwenyezi Mungu na
wakakiandika kitabu kwa mikono yao,
na wakasema kuwa kimetoka kwa Mwenyezi Mungu ili wakiuze kwa thamani ndogo. na
(Qur'an) imeshuhudia uongo wao na kuigeuza kwao haki, basi haiwezekani wakati
huo huo iwaamrishe Waislamu warejee kwao (Mayahudi na Wakristo) katika Mas-ala
wasiyoyajua.
Pili: Bukhari ameeleza katika Sahih yake ndani ya Kitabus-Shahadah
mlango usemao, "Hawaulizwi washirikina". Juzuu ya tatu uk. 163.
Kutoka kwa
Abuhurairah: Amesema Mtume (s.a.w.w.) "Msiwaamini Ahlil-Kitab na wala
msiwapinge (kuwaambia kuwa ni waongo) semeni tumemuamini Mwenyezi Mungu na
yaliyoteremshwa (toka kwake).
Hii inafundisha
kutowarejea (Ahlul-kitab) katika mas-ala na (lililopo) ni kuwaacha na
kuwapuuza, kwa sababu kutowaamini na kisha kutokuwapinga kunakanusha lengo la
kuwauliza ambalo linasubiri jawabu sahihi.
Tatu: Bukhari ameeleza ndani ya Sahih yake katika Kitabut-Tauhidi
mlango wa kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Kila siku yeye yumo katika
mambo." Juzuu ya nane ukurasa 208 kama ifuatavyo:
Kutoka kwa Ibn
Abbas amesema: "Enyi kongamano la Waislamu, vipi mnawauliza Ahlul-Kitab na
hali kitabu chenu alichokiteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mtume wenu (s.a.w.)
ndicho chenye maelezo halisi ya Mwenyezi Mungu na hakikuharibiwa, Mwenyezi Mungu
amekusimulieni kwamba Ahlul-Kitab wamekwisha badilisha na kugeuza (yaliyoteremshwa)
katika vitabu vya Mwenyezi Mungu (vilivyotangulia) wakaandika kwa mikono yao
kisha wakasema hayo ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili wayauze kwa thamani ndogo,
je hajakukatazeni yale yaliyokufikieni katika elimu kuwauliza hao? Basi
fahamuni, namuapa Mwenyezi Mungu; hatujamuona mtu miongoni mwao akikuulizeni
kuhusu yaliyoteremshwa kwenu."
Nne: Lau leo hii tutawauliza Ahlul-Kitab miongoni mwa Wakristo bila
shaka watadai kuwa Isa ni Mungu na Mayahudi wanawapinga (Wakristo kwa madai
hayo) na wala hawamkubali (Isa) japo kwa Utume, na kila mmoja wao anaupinga
Uislamu na Mtume wa Uislamu, na wanasema kuwa (yeye Mtume) ni muongo na ni
mzushi.
Kwa yote hayo
basi haiwezekani ifahamike maana iliyomo katika aya kwamba Mwenyezi Mungu
ametuamrisha tuwaulize wao, na ilipokuwa Ahlud-Dhikr katika dhahiri ya aya ni
wao Ah-Lul-Kitab miongoni mwa Wayahudi na Wakristo, basi hapana shaka hali hii
haikanushi kwamba aya hii imeshuka kwa watu wa Nyumba ya Mtume kama ambavyo
imethibiti kwa
Mashia na Masunni kwa njia sahihi. Kwa hiyo inafahamika kutoka
katika aya hiyo kwamba, Mwenyezi Mungu ameirithisha elimu ya Kitabu ambacho
ndani yake hakuacha kitu kwa hawa Maimamu ambao amewateua kutoka miongoni mwa
waja wake ili watu wawarejee katika Tafsiri na Ta'awiili, na kwa kufanya hivyo
uongofu wao utathaminiwa iwapo watamtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
Kwa kuwa
Mwenyezi Mungu Mtukufu na hekima yake imetukuka alitaka watu wote wawanyenyekee
wateule wanaotoka miongoni mwao, ambao aliwachagua na akawafunza elimu ya
Kitabu ili hali za watu ziwe katika nidhamu. Basi lau watu hawa hawangekuwepo
miongoni mwa watu, nafasi ingekuwa wazi mbele ya wenye kujigamba (kuwa
wanafahamu), na wajinga na hata kila mmoja angefanya kulingana na matamanio
yake na mambo ya watu yangevurugika maadam kila mmoja aweza kudai kuwa ni mjuzi
zaidi kuliko mwingine.
No comments:
Post a Comment