Afrika ya Mashariki imefaidi
mazingira ya amani sana kiasi cha karne mbili zilizopita. Watu wa imani na
itikadi zote waliishi pamoja kwa upendo na mapenzi. Kila mmoja akishiriki
kwenye shughuli za mwenzake za kijamii na za Kidini. Ukiangalia kwenye Jumuiya
za Kiislamu, wote wakihudhuria kwenye Misikiti ya kila mmoja, waliungana pamoja
katika Maulidi na hafla za Muharram, na kupanua ushirikiano wao katika miradi
ya kila mmoja. Kama Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi alivyosema katika
hotuba moja ya hadhara;"Misikiti mingi ya Waislamu wa (Madhehebu ya) Shafi'i
iliyoko Zanzibar na Pemba ilijengwa na kutolewa na Shia Ithna-ashariyya"
Hatimaye
Wahhabi walianza Tabligh (Mahubiri) yao hapa. Badala ya kujaribu kuwaleta
mapagani au wasio waislamu kwenye boma ya Uislamu, nia yao kabisa ilikuwa na
bado inakaziwa katika kuwabadilisha Mashafii wawe Mawahabi. Kwa lengo hili,
hujifanya kama wao ni Masunni, na kuchanganyika pamoja na Masunni. Mawahabi hao
wamepanda mbegu ya fitinana chuki kati ya Madhehebu mbali mbali za
Kiislamu, na hususan kati ya Sunni na Shia. Wanazungumza dhidi ya Shia, na
kusambaza vitabu na vijitabu (vya mambo ya dini) dhidi ya itikadi ya Shia
ambavyo vimejaa mambo ya uwongo na uzushi. Kishawishi chao kiko wazi, kwa
kuwatenganisha Masunni na Mashia, wakitumaini kupata urahisi wa kuingia katika
jamii ya Sunni na Misikiti yao, ingawaje tumaini hili lingali bado kukamilishwa
katika Tanzania.
Hebu tuangalie
katika mzizi wa uovu wa kampeni hii. Huenda hapo nyuma katika mwaka 1979,
ambapo Mapinduzi ya Ki-Islamu yalipotokea katika (nchi ya) Iran, na watawala wa
Kiwahhabi wa Saudia walihadharishwa vikali mno, hata kabla ya tukio la
Mapinduzi ya Kiislamu, wakati Ayatullah al-'uzma al-Khomeini (R.A.) akiwa bado
Najaf (Iraq). Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Saudi Arabia, akizungumza
katika hadhara moja ya Waarabu, aliuonya ulimwengu wa Waarabu kwamba kama
Khomeini ataruhusiwa kuendeleza harakati zake kutoka Iraq kama hapo nyuma, sio
tu kwamba utawala wa Shaha utaangushwa, lakini, hali katika eneo lote vile vile
itakuwa imetibuliwa. Hivyo wakaishinikiza Iraq kuweka vikwazo juu ya Khomeini
kwa hofu ya kwamba, kama juhudi zake zitafanikiwa katika Iran, zitatingisha
tawala zao wenyewe zisizo imara.
Haikushangaza
kwamba mara tu Mapinduzi ya Kiislamu yalipoimarika nchini Iran, hawa Wahhabi
wakaanza propoganda kali yenye chuki dhidi ya Khomeini, dhidi ya Iran na dhidi
ya Ushia. Kalamu za kukodisha zikaanza mchakato kutoa vitabu, makala na
vijitabu dhidi ya Shia. Shia waliitwa Makafiri, na pengine mtu
angeuliza: Kama ni Makafiri, basi kwa nini wanapewa viza kwa ajili ya Hija na
Umra? Wairani waliitwa Majus (Waabudu Moto) kwa nini? Kwa sababu kabla ya kuja
kwa Uislamu waliabudu moto. Kwa hoja hii nasi hatuna haki ya kuwaita
Wahhabi Mushrikina? Kwa sababu kabla ya kuja kwa Uislamu watu wa
Najd walikuwa wakiabudu Masanamu.
Baadhi ya
waajiriwa wao wa ngazi za juu walikuwa ni (marehemu) Ihsan Ilahi Zaheer wa
Pakistan, na Manzoor Ahmad Nu'mani na Abul Hasan Ali Nadwi wa India. Sauti
itokayo kwenye vinywa vyao ni katika watakiwayo na mabwana zao kuyasema, na jambia
la uzayuni lilichovywa kwenye damu ya waislamu linatumika kama kalamu yao.
Kitabu kinachoandikwa dhidi ya Shia na watumwa hawa, kwa miezi michache tu
kinatarujumiwa katika lugha zote kubwa za ulimwengu wa Kiislamu; na hufanywa
kipatikane kila mahali, kadhalika husambazwa bure miongoni mwa Mahujaji:
No comments:
Post a Comment