Baada ya
kuzifuatilia zile Hadithi katika Bukhari, Muslim, na Tirmidhiy huko maktaba ya
chuo chetu,
ulinithibitikia ukweli wa usemi wake, na nilisitushwa na Hadithi zingine zilizo
zaidi ya hizi kwa
dalili za wajibu wa kuwafuata Ahlu-Bayt, jambo lililonifanya niishi katika
hali ya mshtuko. Kwa
nini hatujasikia Hadithi hizi hapo kabla.
Nilizionyesha kwa
baadhi ya wenzangu chuoni ili washirikiane na mimi katika wakati huu
muhimu, baadhi
waliathirika na baadhi hawakujali, lakini mimi niliazimia kuendelea na
uchunguzi hata kama
kufanya hivyo kutanigharimu umri wangu wote. Ilipowadia siku ya
Alhamisi,
nilikwenda kwa Abdul’mun’imu, alinipokea kwa mapokezi mema kwa utulivu na
akasema: “Ni wajibu
juu yako usiharakie na uendelee na utafiti kwa ufahamu wote.”
Kisha tulianza
uchambuzi wa mambo mengine mbalimbali, uliendelea mpaka jioni ya siku
ya Ijumaa,
nilifaidika na mengi na nilivijua vitu vingi ambavyo nilikuwa sivijui, na kabla
ya
kurejea kwangu
chuoni aliniomba vitu vingi nivitafute.
Iliendelea hali
kama hii kwa muda, na hali ya mjadala kati yangu na yeye ilikuwa ikibadilika
kati ya muda na
muda, kwani wakati mwingine nakuwa mkali wa maneno kwake, na
pengine nafanya
inadi kwenye ukweli uliowazi. Kwa mfano nilikuwa ninaporejea baadhi ya
Hadithi katika
vyanzo na ninakuwa na uhakika kuwa ipo, huwa namwambia: “Kwa kweli
Hadithi hizi
hazipo.” Mpaka sasa sijui ni kitu gani kilikuwa kinanisukuma nifanye hivyo ila
ni
kutambua kushindwa
na utashi wa ushindi.
Kwa sura kama hii
na kwa uchambuzi wa ziada mbele yangu ukweli mwingi ulifichuka
mbele yangu ambao
ilikuwa sikuutazamia, na nilikuwa katika muda wote huu nafanya
mjadala sana na
wanafunzi wenzangu, na wenzangu walipoona nawakera waliniomba
nijadiliane na
mwalimu, aliyekuwa akitufundisha Fiq’hi, nikasema: Hapana kizuizi kwangu, lakini tu
kuna vizuizi kati yangu na yeye ambavyo vinanizuia kuwa na uhuru wa kuongea.
Hawakukinaika na
hili, na wakasema: Kati yetu na wewe kuna Ustadh, ukimtosheleza sisi tu
pamoja na wewe.
Nikasema: Mas’ala
sio kutosheka, bali ni dalili na uthibitisho, na kutafuta ukweli. Na katika
somo la kwanza la fiq’hi nilianza
mjadala naye kwa sura ya maswali mengi, nilimuona
hanipingi sana bali
ni kinyume alikuwa anatilia mkazo kuwapenda Ahlul-Bayt (a.s.) na kuwa
kuwafuata na
kuzitaja fadhila zao ni lazima.
Na baada ya siku
nyingi aliniomba niende kwenye maktaba yake kwenye makao ya chuo na
baada ya kwenda
kwake alinipa kitabu chenye juzuu kadha nacho ni (Usul-Kaafiy),
ambacho ni miongoni
mwa vyanzo vya Hadithi vinavyoaminika mno kwa Shia. Aliniomba
nisikipuuze kitabu
hiki kwa kuwa ni turatha ya Ahlu-Bayt. Sikusema kitu kwa shitukizo kama
hili, nilichukua
kitabu na nilimshukuru kwa hilo.
Nilikuwa nakisikia
kitabu hiki na sikupata kukiona, ni jambo ambalo lilinifanya nimshuku
kuwa ni Shia Dr.
huyu, pamoja na kuwa namtambua kuwa ni mfuasi wa Malik, na baada ya
swali na kutaka
tafsiri yake ilinibainikia kuwa yeye ni Sufiy, ni mwenye kujihusisha na
kuwapenda
Ahlul-Bayt (a.s.).
Na wenzangu
walipotambua maafikiano haya kati yangu na huyu ustadh, waliniomba
nifanye mjadala na
ustadhi mwingine aliyekuwa akitusomesha mada ya Hadith, na alikuwa
mtu wa dini sana
mnyenyekevu mwenye tabia njema. Na nilikuwa nampenda sana,
nilikubali ombi
lao, na ilianza kati yetu mijadala mingi, na nilikuwa namuuliza usahihi wa
baadhi ya hadithi,
alikuwa anatilia mkazo kuwa ziko sahihi, na baada ya muda nilihisi
kutopenda kwake na
kutoridhika kwake na mjadala wangu, pia wenzangu walihisi hivyo,
hapo niliwaza njia
bora ya kuendelea na mjadala ni maandishi.
Hivyo basi
nilimwandikia jumla ya Hadithi na riwaya ambazo kwa wazi zajulisha wajibu wa
kufuata madhehebu
ya Ahlul-Bayt (a.s.) na nilimwomba atafiti usahihi wake. Na nilikuwa
namuuliza kila siku
juu ya majibu, naye hutoa udhuru kuwa hajafanya utafiti. Nilimfuatilia
kwa njia hii mpaka
alihisi kuwa namdhiki.
Akaniambia zote ni
sahihi. Nikasema kwa kweli ziko wazi zikihusu wajibu wa kuwafuata
Ahlul-Bayt. Hapo
hakujibu na aliondoka haraka kwenda maktaba.
Mwenendo huu
ulikuwa ni mshitusho kwangu na ni jambo lililonifanya nione ukweli wa usemi
wa Shia. Lakini
nilipenda kwenda polepole na kutoharakia hukumu.
Na miongoni mwa
ajabu ya tukio la bahati ni kwamba mkuu wa chuo naye ni ustadhi Ulwan,
alikuwa
anatusomesha somo la tafsiri, siku moja akasema katika kutafsiri kauli yake ALLAH
(s.w.t):
“Kwa kweli Mtume wa
Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alipokuwa Ghadiir Khum, alinadi kuwaita
watu wakajikusanya,
aliushika mkono wa Ali (a.s.) akasema: “Ambaye mimi ni mtawala
wake hivyo Ali ni
mtawala wake.”
No comments:
Post a Comment