Ni
jambo lililo wazi na lisilopingika kuwa; dini ya Kiislamu mfano wa dini
nyengine ina madhehebu tofauti, na kila dhehebu lina sifa zake katika mambo ya
akida na namna ya utendaji wa amali kutokana na akida hizo wanazoziamini,
lakini tofauti hizo sio kubwa kiasi ambacho pasiwe na uwezekano wa
kutoshirikiana baina ya wafuasi wa dhehebu fulani na wafuasi wa dhehebu jingine,
bali wafuasi hao wa madhehebu tofauti wanaweza kushirikiana na kukabiliana na
fikra za watu wa kimagharibi ili kuondoa kasumba au tata zinazotolewa na watu
hao kwa ajili ya kuiharifu, basi waislamu inawapasa kuihifadhi dini yao na kutowaruhusu watu hao
wenye fikra hizo mbovu kufanikiwa katika malengo yao ya kuiharibu dini hiyo
takatifu.
Kwa hakika kuleta
mashirikiano hayo kunahitajia kutunzwa au kuadhimishwa misingi na vigezo vya
kila madhehebu, na jambo la muhimu zaidi ambalo linafaa kutekelezwa ni kuwa;
kila dhehebu ni lazima litambue akida ya dhehebu jingine, kwa sababu kufanya hivyo kunaweza kuzuia
khitilafu zilizopo baina ya dhehebu na
dhehebu, na kupatikana njia zitakazoweza kuleta mashirikiano.
Njia bora inayoweza
kuyafanya madhehebu kufahamiana ni kutambuana kupitia misingi ya dini yao ya
Kiislamu, na kutambuana akida zao kupitia maulamaa wao maarufu waliobobea kielimu
na wanaotambulika katika jamii, kwa sababu ikiwa watafahamiana akida zao
kupitia wafuasi wa madhehebu yao, wafuasi ambao hawana elimu ya kutosha
inayohusiana na akida zao, na wafuasi wa madhehebu tofauti wakajenga uadui na
kuwekeana chuki kutokana na ikhitilafu walizonazo, hapana shaka uadui na chuki
hizoz itafunga na kuzuia njia zitakazowapeleka katika mashirikiano, na
mafahamiano au mashirikiano yatabadilika na kuwafanya waislamu hao watengane
kutokana na tofauti zao za kiakida na kiamali.
Hivyo ni lazima tujue
akida ya Historia ya kila madhehebu kupitia kwa wenye madhehebu yao badala ya
kujifunza madhehebu Fulani kupitia kwa adui yao. Tukijuana tutaheshimiana na
kupendana kama waislamu.
No comments:
Post a Comment