BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM
Na huu ni mwezi wa Mtume wako bwana wa Mitume wako. Hakika mwezi mtukufu wa Shaaban ni
mwezi mtukufu na mkubwa nao ni mwezi wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) kwani
yeye alisema:
شهر شعبان شهري رحم الله من أعانني على شهري
Mwezi wa Shaabani ni mwezi wangu Mwenyezi Mungu amrehemu
mwenye kunisaidia juu ya mwezi wangu huu).
FADHILA ZA MWEZI WASHAABAN
Kuna habari zilizo pokelewa kutoka kwa Mtume mkarimu
(s.a.w.w) na pia kutoka kwa maimamu waongofu (a.s) zijulishazo kuwa ubora wa
mwezi huu mtukufu na mkubwa ni nyingi sana na malipo ndani ya mwezi huu
ni mara dufu, kwa hakika imekuja na kupolekewa habari kutoka kwa ibnu Abbas ya
kuwa amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) wakati maswahaba wake
walipo kuwa wakizungumzia fadhila za mwezi wa Shaaban mbele yake: Ni mwezi
mtukufu, nao ni mwezi wangu, na wabebaji wa Arshi ya Mwenyezi Mungu wanautukuza
na wanafahamu haki ya mwezi huu, nao ni mwezi ambao huzidishwa ndani yake riziki
za waumini kama ulivyo mwezi wa Ramadhan, na pepo hupambwa ndani ya mwezi huu,
…nao ni mwezi ambao kufanya matendo ndani yake hulipwa mara dufu, jema
moja hulipwa kwa wema sabini, na kosa huanguka na kusamehewa, na madhambi
hughufiriwa, na mema hukubaliwa, na Mwenye nguvu mwenyezi Mungu alie takasika
Huwaelewa ndani ya mwezi huu waja wake, na huwaangali wafungaji wa mwezi
huu na wasimamji kwa ajili ya ibada, na kujifakharisha nao kwa wabebaji wa
Arshi)[1].
Na amesema (s.a.w.w): (Shaaban ni mwezi wenye kutwaharisha,
na Ramadhani ni mwezi wenye kufuta madhambi, ……na Ndani ya mwezi wa Shaaban
huinuliwa matendo ya waja)[2].
No comments:
Post a Comment