Friday, 12 September 2014

ARABIA KABLA YA UISLAMU

Hali ya Kisiasa katika Arabia.
Sura inayoonekana sana ya maisha ya kisiasa ya Arabia kabla ya Uislamu ilikuwa ni kutokuwepo kabisa kwa mfumo wa kisiasa katika muundo wowote ule. Ukiiondoa Yemen iliyoko Kusini Magharibi, hakuna sehemu ya peninsula ya Arabia iliyokuwa na serikali kwa wakati wowote ule, na Waarabu kamwe hawakutambua mamlaka yoyote ile mbali na mamlaka ya machifu wao wa makabila yao. Haya mamlaka ya machifu wa kikabila hata hivyo, yaliegama, kwa namna nyingi, juu ya tabia na nafasi zao, na yalikuwa ya uungwana kuliko kisiasa.
Mwanafunzi wa kisasa wa historia anaona mshangao kwamba Waarabu wameishi, kizazi baada ya kizazi, karne baada ya karne, bila ya serikali ya aina yoyote ile. Kwa vile hapakuwa na serikali, hapakuwa na sheria na utulivu. Kanuni pekee ya nchi ilikuwa ni hali ya uhalifu. Kama inavyotokea, inapofanyika jinai, upande uliodhuriwa ulichukua hatua mikononi mwao, na ukajaribu kupitisha 'hukumu' kwa yule mwovu. Mtindo huu ulisababisha mara nyingi matendo ya ukatili wa kuogofya.
Kama Waarabu walifanya kiasi kidogo cha kujizuia, haikuwa ni kwa sababu ya wepesi wa hisia alizokuwa nazo juu ya maswali ya kweli na batili lakini ni kwa sababu ya kuhofia kuchochea visasi na mauaji ya kurithi kisasi. Mauaji ya kisasi cha kurithi yalimaliza vizazi vizima vya Waarabu. Kwa vile hakukuwepo na vitu kama polisi, mahakama au majaji, ulinzi pekee mtu alioweza kuupata kutokana na maadui zake, ulikuwa katika kabila lake mwenyewe.
Kabila lilikuwa na jukumu la kulinda watu wake hata kama walitenda maovu. Ukabila au 'asabiyya' (moyo wa kiukoo) ulichukua nafasi ya kwanza kabla ya maadili. Kabila lililoshindwa kulinda watu wake kutokana na maadui zao lilijihatarisha kwenye kebehi, kashfa na dharau. Maadili, kwa kweli hayakuingia kwenye picha mahali popote pale. Kwa vile Arabia haikuwa na serikali; na kwa vile waarabu walikuwa na utawala huria kwa silika yao, walifungana katika mapigano yasiyokwisha. Vita ilikuwa ni desturi ya kudumu ya jamii ya kiarabu. Jangwa liliweza kuchukua idadi ndogo tu ya watu, na hali ya vita vya kikabila ilidumisha uthibiti mkali juu ya ongezeko la watu. Lakini Waarabu wenyewe hawakuiona vita katika mwanga huu. Kwao wao, vita vilikuwa burudani au kiasi mchezo wa hatari, au aina ya tamthiliya ya kikabila, iliyofanywa na wenye weledi (ubingwa), kwa mujibu wa mfumo wa kanuni za zamani na ushujaa, ambapo "watazamaji" walishangilia.
Amani ya kudumu haikuwa na mvuto kwao na vita vilitoa fursa ya kukwepa kazi ngumu na kutokubadilika kwa mwenendo wa maisha katika jangwa. Wao kwa hiyo walichochea msisimko wa mapambano ya silaha. Vita viliwapa fursa ya kuonyesha vipaji vyao katika kutupa mishale, ufundi wa kurusha panga na upandaji wa farasi, na pia, katika vita, wangeweza kujipatia sifa kwa ushujaa wao na wakati huohuo kuleta fahari na heshima kwa makabila yao. Kwa mara nyingi, Waarabu walipigana ili kupigana tu, ama iwepo au isiwepo sababu ya kuchochea vita.
Kwa bahati mbaya mpaka leo kuna baadhi ya watu wanaojifanya waislamu wamekuwa na tabia za kupenda vita na kuuwa watu kama ilivyokuwa kabla ya Uislamu. Uislam haujafanikiwa kuwakomboa watu hawa wenye uchu wa kumwaga damu ya waislamu. Kiongozi wa wamwaga damu hawa ni Muhammad ibn Abdul-wahhab aliyeirithi tabia hii mbaya toka kwa Ibn Taimiyyah na Maswahhaba waovu kama Khalid ibn Walid

No comments:

Post a Comment