Friday 12 September 2014

UTAFITI ULIONIFANYA NIWE MSHIA ITHNAASHARIYYAH

Ilikuwa kutafuta utaratibu na fikra iliyowiva na taaluma itakiwayo ni vigumu, na daraja hii
ilikuwa chungu, japokuwa utafiti wangu ulikuwa kwa sura ya msamaha na wa kimaumbile.
Katika maisha yangu ya kawaida nilikuwa nauliza na kujadili na vinginevyo, wala hapakuwa na utayarifu wa kutafiti na kuhimili. Na baada ya uvamizi mkali wa mawahabi kuivamia Sudan, na kushika kasi malumbano na mijadala na kukithiri kwa harakati za kidini, ukweli mwingi ulifichuka, na zikajitokeza tofauti na mifarakano mingi ya kihistoria, kiitikadi na kifiq’hi.
Na tendo la kuvikufurisha baadhi ya vikundi na kuvitoa nje ya tanzi la uislamu ilianza, ni
miongoni mwa mambo ambayo yalisababisha mfarakano wa kimadhehebu na safu
kutengana. Pamoja na uchungu wa yaliyotokea, nilipata utashi wangu na udadisi wangu
ulizidi, na nilikuwa naona uhalisi wa yale maswali yaliyokuwa yanaishawishi akili yangu.
Hapo basi hima yangu ya kuutilia maanani uwahabi ilizidi, nilikuwa nafuatilia mijadala yao na mikusanyiko yao ambayo ilikuwa inanifunga mimi. Na ambalo ni la muhimu nililojifunza kutoka kwao katika ngazi ile, ni ujasiri na kuukabili ukweli na kuukinza, nami nilikuwa naamini kuwa ukweli ni kitu kitakatifu na ni mwiko kuuhujumu au kuupinga, japokuwa uangalizi wangu ulikuwa mwingi kuuhusu, ambapo aghlabu nilikuwa siangalii kupitia dhati yangu na umbile langu, hivyo basi nilikuwa najizuia sana matendo na zoezi za jamii ya kidini.
Niliendelea nao, na ilijiri kati yangu na wao mijadala mingi, ambayo ukweli wake ulikuwa
yale maswali ambayo yalikanganya akili yangu, baadhi yake nilipata majibu yaliyoniridhisha katika ngazi ile, na kulikuwa na maswali sikupata majibu yake kutoka kwao, hilo lilikuwa dhamana tosha kwangu kuwaelemea na niwaunge mkono, japokuwa kulibaki baadhi ya mazingatio ambayo yalikuwa kizuizi kati yangu na kujihusisha moja kwa moja na mwendo wa kiwahabi.
La kwanza na la muhimu ni kuwa mimi sikupata kwao nitoshekalo nalo,
ambalo laweza kuwa jibu la matamanio yangu ya kiujumbe. Na wakati mwingine wasiwasi ulikuwa unanichukua kwa kauli yake: Kwa kweli unalolifikiria na kulitafiti ni kitu cha mfano tu hakina ukweli, na uwahabi ni sampuli bora ya uislamu na hapana kitu badala yake….
Nilikuwa nasukumwa na wasiwasi huu na kuusadiki kwa kutokuwa kwangu na maarifa na fikra za vyuo vingine, lakini haraka nilikuwa nang’amua kuwa ambalo Jamaludin amelifanya haiwezekani liwe ndio hii fikra ya kiwahabi. Kwa hiyo nilikuwa nasema waziwazi: Kwa kweli Uwahabi ni njia ilio karibu mno kuelekea Uislam, kwa sababu yale wayafanyayo kuonyesha dalili, na matamko rasmi ya kisheria ili kuthibitisha ukweli wa madhehebu yao, ni jambo ambalo sijaliona katika vikundi vingine humu (nchini) Sudan.
Lakini tatizo lao ni kuwa madhehebu hii waliojijengea yashabihiana mno na kanuni za
hisabati, kwani yenyewe ni desturi na kanuni iliyoganda, hutekelezwa bila ya kuwa na akisi ya kimaendeleo iliyo wazi katika maisha ya mwanadamu. Na katika fani ya kuamiliana na dunia hii katika nyanja tofauti za mtu mmoja au za kijamii au ya kiuchumi au kisiasa… na hata jinsi ya uhusiano na Mwenyezi Mungu (s.w.t).
Bali ni kinyume kabisa mara nyingi humfanya mtu awe mkiwa mwenye kujitenga mbali na jamii, kwa aliyonayo miongoni mwa ufinyu wa fikra katika kila mikato yake. Mtu miongoni mwao hawezi kuishi na jamii bali huwa ni mwenye kujipambanua mbali nao kwa vazi lake na mwenendo wake na katika kila sehemu ya maisha yake, na hata jinsi ya uongeaji wake, hazoeani ila na watu wa aina yake.
Nilikuwa nahisi kuwa wameghurika na wenye kiburi na dharau kwa kuwa wao huwaangalia watu wengine wakijiona wao wako juu, hawana maingiliano nao wala hawashirikiani nao katika maisha yao.
Vipi watashirikiana nao?! Hali kila lifanywalo na jamii ya kiislamu kwao ni bidaa na
upotovu. Mimi nakumbuka vyema ulipoingia mvuto wa kiwahabi kijijini petu katika muda
mfupi na bila ya darasa lolote wala uelewa, kundi kubwa la vijana walijiunga kwenye
uwahabi, hawakuendelea muda mwingi wote walijitoa, na hili lilikuwa ndio tazamio langu,
kwa sababu madhehebu mpya imewazuia kuchanganyika na jamii na iliwaharamishia
kawaida nyingi ambazo walilelewa nazo, hali zikiwa haziendi kinyume na dini.
Na jipya nikumbukalo ni kuwa, miongoni mwa vitu ambavyo vijana waliojiunga na uwahabi walikuwa wanataabika navyo, ni kwamba ilikuwa ni kawaida kijijini petu vijana zama za usiku wa mbaramwezi hujumuika na kuketi kwenye mchanga ulio safi wanapitisha wakati wao huko, nao ni wakati pekee wa kuonana vijana wa kijijini ambao wanafanya kazi mchana kutwa katika mashamba yao na katika shughuli zao walizozizoea, basi Sheikh wao alikuwa anawazuia kufanya hivyo na kuwaharamishia tendo hilo kwa hoja ya kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) ameharamisha kukaa njiani, japokuwa sehemu hizi hazizingatiwi kuwa ni njia

No comments:

Post a Comment