**Mtume(S.A.W) amesema :" haki za muislam juu ya waislamu (wenzake) ni sita(6) ; Kumtembelea mgonjwa, kukubali mialiko, kumsaidia mwenye kuonewa(kudhulumiwa), kutimiza kiapo ,kurudisha (kujibu) salamu na kumjibu mwenye kupiga chafya na anapokufa kufuata (kuhudhuria) shughuli za mazishi." (Muslim).
(1) KUSALIMIA NA KUJIBU SALAMU :
** Kusalimiana ni moja ya njia za kueneza mapenzi baina ya waislamu na njia ya kuingia peponi . Mtume (saw) amesema :" Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake , hamtaingia peponi mpaka muamini na hamtoamini mpaka mpendane . Je nisiwaelekeze (niwambie) kitu ambacho mkikifanya mtapendana? Sambazeni maamkizi yaamani (assalamu alaykum) miongoni mwenu."(MUSLIM).
**Pia "Assalamu alaykum" ndio maamkizi ya watu wa peponi. Allah(S.W) anasema:" Na waliomcha Mola wao mlezi wataongozwa kuendea peponi kwa makundi, mpaka watakapoifikia, nayo milango yake imekwisha funguliwa . Walinzi wake (wa milango ya peponi) watawaambia "SALAAM ALAIKUM,(amani iwe juu yenu. Mmetwahirika( mmefanya vyema). Basi ingieni humu mkae milele."(39:73).
**Allah anatuamrisha turudishe salamu sawa au iliyobora zaidi, "Na mnapoamkiwa kwa maamkizi yoyote, basi itikieni kwa yaliyobora kuliko hayo, au rejesheni hayo hayo...."(4:86).
(2) KUMJIBU MWENYE KUPIGA CHAFYA;
**Mtume (SAW) amesema," Ikiwa yeyote kati yenu akipiga chafya, nilazima aseme "AL-HAMDULILAH"(sifa zote njema ni za Allah, na ndugu yake(muislamu) au mwenzake aseme," YAR-HAMUKA- LLAH" (rehma za Allah ziwe juu yako). Mpigaji chafya akisema"yar-hamuka-llah", wenzake waseme,"YAHDIKUMUL-LLAH WA YUSLIH BALAKUM"(Allah akuongoze na aimarishe hali yako) .
Hivyo mpigaji chafya na mwenye kujibu watapata barka za dua. Mtume (saw) alikua akifunika uso wake kwa mkono au nguo na akishusha sauti yake wakati akipiga chafya.( al-tirmidhee).
(3) KUMTEMBELEA MGONJWA:
** Ali bin Abu Talib(ra) ameripoti :"Nimemsikia mtume wa Allah(saw) anasema:" Wakati muislamu akimtembelea muislamu mgonjwa alfajiri, malaika elfu sabiiini(70,000) huendelea kumsalia (mtembeleaji) mpaka jua likichoomoza. Ikiwa atamtembelea jioni,malaika elfu sabiini(70,000) huendelea kumsalia (mtembeleaji) mpaka asubuhi. Na(ujira wake) atavuna (atakua) matunda ya peponi."(at-tirmidhee).
**Pia mtume (saw) amesema,"Wakati muislamu anapomtembelea ndugu yake muislamu mgonjwa, atakua katika bustani za peponi mpaka atakaporudi."MUSLIM).
(4) KUHUDHURIA SHUGHULI ZA MAZISHI:
**Mtume wa Allah(saw) amesema,"Yeyote atakaye msindikiza maiti mpaka akamsalia(sala ya maiti), atapata thawabu (malipo)sawa na QIRAT moja, na yeyote atakayemsindikiza maiti mpaka akazikwa, atapata thawabu (malipo) sawa na QIRAT mbili". Ikaulizwa QIRAT ni nini?" akajibu " ni kama milima miwili mikubwa (sana)".
(5)KUMSAIDIA MUISLAMU KATIKA HAKI(UKWELI):
**Mtume(saw) amesma:"Msaidie ndugu yako(muislamu), aidha ni muonevu
(dhaalimu) au mwenye kuonewa(mwenye kudhulumiwa). Watu wakauliza," O mjumbe wa Allah ni sawa kwa wenye kuonewa (kudhulumiwa), lakini vipi tumsaidie akiwa ni muonevu (dhaalimu)?" Mtume(saw) akasema" ni kumuepusha kuonea(kudhulumu) wengine,"(BUKHARI).
(dhaalimu) au mwenye kuonewa(mwenye kudhulumiwa). Watu wakauliza," O mjumbe wa Allah ni sawa kwa wenye kuonewa (kudhulumiwa), lakini vipi tumsaidie akiwa ni muonevu (dhaalimu)?" Mtume(saw) akasema" ni kumuepusha kuonea(kudhulumu) wengine,"(BUKHARI).
Kutokana na hadithi hii kuna maana mbili za kumsaidia muislamu aliyedhulumiwa.
(1)KUMSAIDIA MWENYE KUONEWA (kudhulumiwa) ;
**Kwa kusimama mbele ya muonevu(dhaalimu) kadri ya uwezo wetu na kumsapoti(ALIYEONEWA) iwe kwa uhai,pesa au dua mpaka arudishiwe haki yake .
**Kuna malipo makubwa katika hili. Mtume(saw) amesema :"Allah humsaidia mja wake madamu tu mja (huyu) humsaidia ndugu yake muislamu".(MUSLIM).
**Pia Mtume(saw) amesema, "Muislamu ni ndugu wa muislamu mwenzake, hivyo asimuonee(asimdhulumu), wala asimkamatishe(asimkabizishe) kwa muonevu(dhaalimu).Yeyote mwenye kumtimizia (kumtatulia) mahitaji ya ndugu yake (muislamu), Allah atamtimizia (atamtatulia) mahitaji) yake.
Na yeyote mwenye kumuondolea yasiyomridhisha(matatizo,ugumu,shida nk) ndugu yake (muislamu), Allah atamuondolea yasiyomridhisha(adhabu nk) siku ya kufufuliwa,na yeyote mwenye kumsitiri muislamu,Allah atamsitiri siku ya kufufuliwa.".
** Hivyo tuwasaidie na kuwasapoti ndugu zetu waislamu waliodhulumiwa kwa kuwalinda wao,haki zao na heshima zao.
Pia kwa kuwapa pesa na sadaka kwa kuwasapoti na kuwatia nguvu wakati wa shida au kuwaombea dua kwa siri Allah awasaidie na awaondolee shida zao.
Mtume(saw) amesema, "Muislamu yeyote anayemuombea muislamu mwenzake kwa Allah kwa siri, malaika atasema hivyo hivyo iwe juu yako."(MUSLIM).
Mtume(saw) amesema, "Muislamu yeyote anayemuombea muislamu mwenzake kwa Allah kwa siri, malaika atasema hivyo hivyo iwe juu yako."(MUSLIM).
(2)KUMSAIDIA MUISLAMU MUONEVU(DHAALIMU);
**Ni kwa kusimama mbele yake na kumuepusha na kumzuia na kumuombea dua ALLAH amuongoze katika njia ya haki. HII ni sawa na kuilinda jamii nzima(waislamu ) na kusababisha kupatikana usalama, uadilifu, usawa, utulivu na amani, pia kuepukana na uharibifu na madhara.
**ALLAH anasema:" Na ikiwa makundi mawili kati ya waumini wanapigana, basi yapatanisheni. Na ikiwa moja ya hao linamdhulumu mwenzie , basi lipigeni linalodhulumu mpaka lirejee katika amri ya Allah. Na likirudi basi yapatanisheni kwa uadilifu..."( 49:9)
********** NA ALLAH NDIE MJUZI ZAIDI *******************
No comments:
Post a Comment