Tuesday 9 September 2014

ANSWARU SUNNAH, UWAHHABI, USALAFI NA TAUHID

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Je, kuna muumba asiyekuwa Mwenyezi Mungu" Qur'an, 35:3
Na Amesema tena:
"Waambie, Mwenyezi Mungu ndiye muumba wa kila kitu"Qur'an, 13:16.
Umma umekubaliana juu ya Tauhidi yake katika Rububiya yake na kwamba hapana Mola wala mwenye kusimamiya (mambo yao) asiyekuwa yeye.
Amesema Mwenyezi Mungu:
Yeye ndiye anayesimamia mambo yote hakuna muombezi ila baada ya idnini yake, huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu basi muabuduni yeye, Je, hamna kumbukumbu?
Pia wamekubaliana kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika Ibada na kwamba, yeye Mwenyezi Mungu ndiye Mola ambaye anastahiki kuabudiwa na hakuna wa kuabudiwa asiyekuwa Yeye.
Mwenyezi Mungu Amesema:
"Waambie, Enyi mliopewa Kitabu, njooni kwenye neno lililo sawa kati yetu na ninyi ya kwamba, tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, na wala tusimshirikishe na chochote, wala baadhi yeta tusiwafanye kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu".
Qur 'an, 3:64
Bali hizi ndizo nukta ambazo zenye kuafikiana baina ya sheria zote za mbinguni, na yote haya yanaonekana kuwa ni miongoni mwa mambo ya kipekee kwa baadhi ya wafuasi wa sheria zilizopita. Basi mtazamo ulio kinyume na misingi hii ni miongoni mwa vitendo vya uchafuzi na kupotosha vinavyotokana na wanachuoni, Watawa na Makasisi (wao).
Cha ajabu, (na midhali u-hai utaona maajabu zaidi) in kwamba, Uwahabi unatokana na fikia ya Sheikh mpotofu aitwaye Ibn Taimiyyah ambaye ametuarifisha maana ya Tauhidi katika kitabu chake aliposema: "Hakika Mwenyezi Mungu yuko juu ya mbingu yake kwenye arshi yake, yuko juu ya viumbe wake"
Na amesema tena: "Mola wetu hushuka mpaka kwenye mbingu ya dunia kila siku inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku kisha husema; Nani ataniomba (saa hizi) nami nitamkubalia (maombi yake) nani ataniomba nami nitampa, ni nani atanitaka msamaha nami nitamsamehe".
Haya ndiyo maarifa ya mtu huyo (Ibn Taimiyyah) na huku ndiko kumtakasa kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu na (yote haya aliyoyasema) inajulisha wazi kabisa kuwa yeye anaitakidi kuwa Mwenyezi Mungu anao mwili na anapatikana upande fulani. Na (huyu Ibn Taimiyyah) amesema hayo kutokana na kung'ang'ania kwake dhahiri ya aya na hadithi za Mtume bila ya kuzitafiti kwa undani aya zilizokuja kuhusu maudhui hiyo, na bila ya kufanya uhakiki katika isnadi za hadithi na madhumuni yake.
Basi iwapo haya ndiyo maoni ya mwalimu (wa Mawahabi) basi itakuwaje hali ya watu wanaoramba vikombe vyake na wanakaa katika meza zake kama kina Ibn Al-Qayyim na Muhammad bin Abdul-Wahhab. Na cha ajabu ni kwamba, hawa nao wanataka wawe ni waalimu wa Tauhidi na walinganiaji wa Tauhid. Na Mwenyezi Mungu amrehemu mshairi aliyesema: "Katika maajabu ya duniani ni kwamba, mwenye ugonjwa wa manjano anadai kuwa ni mganga na mwenye macho mabovu awe mwenye kutengeneza dawa ya macho na kipofu awe mnajimu, na msomaji wetu wa Qur'an awe Mturuki na Khatibu wetu awe Muhindi, basi njooni tulie na tupige vifua juu ya Uislamu, (Tuulilie kwa msiba uliyoufika).
Rejea:
Maj-mu'a 'Tur-Rasailil-Kubra, cha Ibn Taimiyyah, Al-A'qidatul-Wasitiyah uk. 401.

No comments:

Post a Comment