Friday, 12 September 2014

MASHIA NI AKINA NANI,AU NINI MAANA YA SHIA?

Assalaam alaikum:
MASHIA NI AKINA NANI,AU NINI MAANA YA SHIA?:
Shia ni jina amabalo huitwa wale watu wa dhehebu la waislaam ambao hujulikana kihistoria kama "شيعة علي" = SHIAT ALI = "MASHIA WA ALI" yaani (wafuasi wa Ali) au "أتباع علي" = (Wafuasi wa Ali).
Na mara nyingi Istilahi hii inapotajwa huashiria MASHIA AMBAO NI WAFUASI WA MAIMAM KUMI NA WAWILI, na katika Mashia hili ndilo kundi kubwa zaidi ukilinganisha na mashia wengine ambao si wafuasi wa Maimam Kumi na wawili kama mashia wale wanaoitwa Zaidiyya, na Ismailiyya, hawa pia ni Mashia lakini si mashia wenye kufuata Maimam Kumi na wawili bali ni mashia ambao wanaishia kwa Zaidi na Ismaili na ndio maana wakanasibishwa kwa majina hayo wakaitwa Zaidiyya na Ismailiyya.
Hivyo tunaposema Mashia hatumaanishi au kukusudia Mashia Zaidiyya wala Mashia Ismailiyya, bali tunamaanisha wale Wafuasi (Mashia) ambao hufuata Maimam Maasumin Kumi na wawili kutoka katika Kizazi Kitukufu cha Mtume (s.a.w.w) na ambao ndio walioteuliwa na Mtume (s.a.w.w) kuwa Makhalifa na Mawasii baada yake kwa dalili zilizowazi ndani ya vitabu vya kishia na kisunni.
Hivyo: Mashia hawa au wafuasi hawa kwa kuwa wanafuata Maimam 12 wa Ahlul-bait (a.s) ndio maana wakaitwa SHIA ITHNA ASHARI, kwa maana MASHIA au WAFUASI WENYE KUWAFUATA MAIMAM KUMI NA WAWILI.
Na Maimam hao kumi na wawili (12) watwaharifu (a.s) majina yao yametajwa katika Hadithi za Mtume (s.a.w.w) na riwaya mbalimbali zilizopokelewa kwa pande zote mbili au kwa Madhehebu zote mbili yaani: Shia Ithna Ashari na Ahlu Sunna.
Kundi hili la Mashia wenye kuwafuata Maimamu kumi na wawili katika Mashia ndio lenye wafuasi wengi zaidi ukilinganisha na makundi mengine.Hivyo kutokana wingi wa wafuasi wake ndio maana mara nyingi likitajwa neno SHIA basi bongo za watu hujua kuwa wanaokusudiwa ni Mashia Ithna Ashari yaani: WAFUASI WA MAIMAM KUMI NA WAWILI (A.S). Ndio ni neno, la jumla lakini kutokana na wingi wa wafuasi wa Maimam Kumi na wawili neno hilo likitajwa moja kwa moja linawahusu hao wenye kuwafuata Maimam kumi na wawili.
Lakini waliowachache tunaweza kusema hawajui ufafanuzi huu, bali wao wanachokijua ni kundi la Shia, hawajui kuwa Shia ni kama Bahari, maana ukisema bahari lazima uainishe unakusudia bahari ipi, maana kuna bahari ya Hindi, kuna bahari ya Atlantiki, kuna bahari ya Pasific... hivyo ni bora -ikiwa hatutasema ni lazima- ueleweke unakusudia bahari ipi!. Ndio unasema Bahari, lakini bahari ipi umelenga kuikusudia katika katika mazungumzo yako. Na hivyo hivyo kuhusu Shia, ukisema shia unaeleweka umesema Shia, lakini hueleweki umekusudia shia wepi hivyo ni bora useme Shia zaidiyya au Shia Ismailiyya au Shia Ithna Ashari, kama unavyosema Bahari ya hindi, Bahari ya Pasific, na Bahari ya Atlantiki!.

4 comments:

  1. Na hii (s.a.w.w) shekhe umeitoa wap mana,me,najua,ina andikw hiv (s.a.w)

    ReplyDelete
    Replies
    1. (S.a.w.W) ebu itamke herefi mojamoja utapata majibu yako

      Delete
    2. S.a.w.w
      SwallAllah alayh waalih wasallam

      Delete
    3. S.A.W.W.....salallau alay waali wasalam

      .ama

      Salallau alehi Walaali wa Salam

      Delete