Friday, 12 September 2014

MOHAMMAD (S.A.W.W) AITWA MKWELI MWAMINIFU

MOHAMMAD (S.A.W.W) AITWA MKWELI MWAMINIFU
Mapema katika maisha, Muhammad, nabii alijenga sifa ya ukweli, uaminifu na maamuzi yenye busara. Kwa vile hakukuwa na mabenki siku zile, alikuja kuwa "benki" ya watu wa Makka. Walileta fedha zao, mapambo ya vito, na vitu vinginevyo vya thamani kwake kwa uhifadhi wa salama, na wakati wowote walipotaka kurudishiwa kitu chochote, aliwarudishia. Walimuita yeye al-Amin (Mwaminifu) na as-Sadiq (Mkweli).
"Kwa kujaaliwa na akili safi adilifu na tamaa dhaifu, mkimya na mwenye mazingatio, yeye (Muhammad) aliishi zaidi kiupweke, na tafakari ya moyoni mwake ilimpatia shughuli kwa masaa ya mapumziko yaliyotumiwa na watu wenye tabia duni katika michezo ya kikatili na ufisadi. Tabia njema na muelekeo wa heshima wa kijana huyu asiyejionyesha vilimletea kukubalika kwa wananchi wenzie; na alipata lile jina, kwa kuafikiana kwa jumla, la Al-Amin, 'mwaminifu.' Hivyo aliheshimiwa na kutukuzwa, Muhammad aliishi maisha ya utulivu na ya kitawa katika familia ya Abu Talib." (The life of Muhammad 1887, uk 20).

No comments:

Post a Comment