Friday 12 September 2014

HOTUBA ALIYOITOA MTUME (S.A.W.W) ALIPOKUWA GHARIR KHUM.

"………. Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kuwakamilishieni neema yangu kwenu, na nimewaridhieni kwamba Uislamu ndiyo dini yenu." (Q:5:3). Baada ya Khutuba yake Mtume (s.a.w) alimtaka kila mtu kula kiapo cha utii kwa 'Ali (a.s) na kumpongeza. Miongoni mwa waliofanya hivyo ni Umar bin al-Khattab, ambaye alisema: "Hongera Ali Ibn Abi Talib! Leo umekuwa bwana wa waumini wote wanaume na wanawake."
Mwarabu mmoja aliposikia tukio la Ghadir Khum, alikuja kwa Mtume (s.a.w) na akasema: "Ulituamrisha tushuhudie kwamba hakuna mungu isipokuwa Allah na kwamba wewe ni Mjumbe wa Allah, tumekutii. Umetuamrisha kusali sala tano kwa siku, tukakutii.Umetuamrisha kufunga (saumu) mwezi wa Ramadhani, tumekutii. Kisha umetuamrisha kwenda kuhiji Makka tukakutii. Lakini hukutosheka na yote haya yote ukamnyanyua binamu yako kwa mkono wako na ukamuweka juu yetu kama mtawala kwa kusema 'Ali ni mawla wa yule ambaye mimi ni mawla kwake: je, amri hii yatoka kwa Allah au yatoka kwako wewe?"
Mtume (s.a.w) akasema: "Kwa jina la Allah ambaye ndiye Mola Pekee! Haya yanatoka kwa Allah, Mwenye nguvu na Mtukufu" Aliposikia jibu hili aligeuka na kuelekea aliko ngamia wake jike huku akisema: "Ewe Allah! Kama asemayo Muhammad ni sawa, basi vurumisha jiwe juu yetu kutoka angani na tupatie sisi adhabu kali na mateso." Kabla hajamfikia ngamia wake Allah alimvurumishia jiwe ambalo lilipiga juu ya kichwa chake na kupenyeza ndani ya mwili wake na kumuacha akiwa amekufa. Ni katika tukio hili kwamba Allah (swt) aliteremsha aya ifuatayo:
"Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea. Kwa makafiri hapana awezaye kuizuia. Kutoka kwa Allah, Mola wa mbingu za daraja." (Qur'an 70:1-3) :
Wengi wa wanachuoni hawa hawakunukuu tu tangazo hili la Mtume (s.a.w) bali vile vile wanaliita sahihi: " al-Hakim al-Naysaburi, al-Mustaddrak 'ala al-Sahihyn (Beirut), juzuu 3, uk. 109-110, uk. 133, uk. 148, uk. 533. Ameelezea kwa uwazi kwamba hadithi hii ni sahihi kwa mujibu wa vigezo vya Bukhari na Muslim. al-Dhahabi alithibitisha hukumu yake.
" al-Tirmidhi, Sunan, (Cairo), juzuu 5, uk. 633.
" Ibn Majah, Sunan, (Cairo, 1952), juzuu 1, uk. 45.
" Ibn Hajar al-'Asqalani, Fath al-Bari bi Sharh Sahih al-Bukhari, (Beirut, 1988), juzuu 7, uk. 61.
" al-'Ayni, 'Umdat al-Qari Sharh Sahih al-Bukhari, juzuu 8, uk. 584.
" al-Suyuti, al-Durr al-Manthur, juzuu 2, uk. 259 na uk. 298.
" Fakhr al-Din al-Razi, Tafsir al-Kabir, (Beirut, 1981), juzuu 11, uk. 53.
" Ibn Kathir, Tafsir Qur'an al-Adhim, (Beirut) juzuu 2, uk. 14
" al-Wahidi, Asbab al-Nuzu, uk.l64.
" Ibn al-Athir, Usd al-Ghaba fi Ma'rifat al-Sahaba, (Cairo, 1932), juzuu 3, uk.92.
" Ibn Hajar al-'Asqalani, Tahhdib, (Hyderabad, 1325), juzuu7, uk. 339.
" Ibn Kathir, al-Bidayah wa al-Nihayah, (Cairo, 1932), juzuu7, uk. 340, juzuu 5, uk. 213.
" al-Tahawi, Mushkil al-Athar, (Hyderabad, 1915), juzuu 2 uk. 308-9.
" Nur al-Din al-Halabi al-Shafi'i, al-Sirah al-Halabiyya, juzuu3, uk. 337.
" al-Zrqani, Sharhe al-Mawahib al-Ladunniyya, juzuu 7, uk. 13

No comments:

Post a Comment