Friday 12 September 2014

MASHIA NI WATEKELEZAJI WA AMRI ZA MTUME MOHAMMAD (S.A.W.W)

Mashia wanatekeleza amri ya Mtume (s.a.w.w) inayosema: "Nimekuachieni vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Kizazi changu, vitu ambavyo mkishikamana navyo kamwe hamtapotea baada yangu." Kama ambavyo zinashuhudia Sihah za Sunni ukiachilia mbali vitabu vya Kishia.
Badala ya kuwashukuru (Mashia) na kuwatanguliza na kuwaboresha juu ya wengine kwa kufuata kwao maamrisho ya Mtume (s.a.w.w.), tunawashutumu na kuwakufurisha na kujitenga nao, jambo hili siyo uadilifu wala haliingii akilini.
Mimi na mashia wote tunapinga kauli za kijinga na za uongo ambazo haziwezi kusimamisha dalili wala hoja na hazina uzito kwa wanataaluma miongoni mwa watoto wa umma wetu kwamba, "Eti Mashia wanayo Qur'ani yao, au eti wao wanasema kwamba aliyepewa Utume ni Ali, au kwamba Abdallah ibn Sabaa' Myahudi ndiye muanzilishi wa Ushia."Na mengineyo miongoni mwa kauli dhaifu ambazo Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa hayo ni miongoni mwa uzushi wa maadui wa Uislamu na maadui wa Ahlul-Bait na wafuasi wao. Na hayo ni mambo hayakuzushwa isipokuwa ni kutokana na ubinafsi mpotovu na ujinga wenye kero iliyopita kipimo

No comments:

Post a Comment