Friday, 12 September 2014

WAULIZENI WENYE KUMBUKUMBU IKIWA NINYI HAMJUI (QUR. 16:43 NA 21:7)

WAULIZENI WENYE KUMBUKUMBU IKIWA NINYI HAMJUI (QUR. 16:43 NA 21:7)
Bila shaka aya hii Tukufu inawaamuru Waislamu kuwarejea watu wenye kumbukumbu kwa kila linalowatatiza ili wapate kuufahamu muelekeo ulio sawa, kwani Mwenyezi Mungu amewaandaa (wenye kumbukumbu) kwa ajili hiyo baada ya kuwafunza, basi wao ndiyo waliobobea katika elimu na ndiyo wanaofahamu Ta'wili ya Qur'an.
Kwa hakika aya hii ilishuka kuwatambulisha Ahlul-Bait (a.s.) nao ni Mtume Muhammad, Ali, Fatma, Hasan na Husein, na hili lilitendeka katika zama za Mtume. Amma baada ya Mtume (s.a.w.w.) mpaka kitakaposimama Qiyama (wenye kumbukumbu) ni hawa hawa watano waliotajwa ambao ndiyo Ahlul-Kisaa na huongezwa kwa hao, Maimamu tisa kutoka katika kizazi cha Hussein (a.s.) ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu amewabainisha katika Minasaba mbali mbali na akawaita kuwa ni Maimamu wa uongofu na ni taa ziondoazo kiza na wao ndiyo wenye kumbukumbu, na ndiyo waliobobea katika elimu, Mwenyezi Mungu amewarithisha elimu ya kitabu.
Riwaya hizi zimethibiti na ni sahihi tena mutawatir kwa Mashia tangu zama za Mtume (s.a.w.w.), na wamezieleza baadhi ya wanachuoni wa Kisunni, na wafasiri wao wamekiri kwamba kushuka kwa aya hii kunawahusu Ahlul-Bait (a.s.). Ninawataja miongoni mwa wanachuoni hawa kwa kutolea mfano:
1) Im1)Imam Thaa'labi katika Tafsiri yake (alipozunhumzia) maana ya aya hii katika Surat An-NahliNahl.
3) Tafsirul-Qur'an ya ibn Kathir Juzuu ya pili ukurasa 570570.
3) Tafsirut-Tabari, Juzuu ya kurni na nne ukurasa 109.
4) Tasirul-Alusi iitwoyo Ruhul-Maani Juzuu ya kumi na nne ukurasa wa 134.
5) Tafsirul-Qurtubi Juzuu ya kumi na moja ukurasa 272.
6) Tafsirul-Hakim iitwayo Shawa-Hidut-Tanzil, Juzuu ya kwanza ukurasa 334.
7) Tafsir At-Tustari, itwayo Ih-QaaQul-Haq, Juzuu ya tatu ukurasa 482.
8) Yanahi'ul-Mawaddah cha Al-Qanduzi Al-Hanafi ukurasa wa 51 na 140.
Na ilivyokuwa wenye kumbukumbu kwa dhahiri ya aya ni Ahlul-Kitab miongoni mwa Mayahudi na Wakristo, basi imetulazimu juu yetu kubainisha wazi kwamba wao sio waliokusudiwa katika aya hiyo Tukufu.
Kwanza; Kwa sababu Qur'an Tukufu imewataja (Mayahudi na Wakristo) mara nyingi katika aya nyingi kwamba wao waliyageuza maneno ya Mwenyezi Mungu na wakakiandika kitabu kwa mikono yao, na wakasema kuwa kimetoka kwa Mwenyezi Mungu ili wakiuze kwa thamani ndogo. na (Qur'an) imeshuhudia uongo wao na kuigeuza kwao haki, basi haiwezekani wakati huo huo iwaamrishe Waislamu warejee kwao (Mayahudi na Wakristo) katika Mas-ala wasiyoyajua.
Pili: Bukhari ameeleza katika Sahih yake ndani ya Kitabus-Shahadah mlango usemao, "Hawaulizwi washirikina". Juzuu ya tatu uk. 163.
Kutoka kwa Abuhurairah: Amesema Mtume (s.a.w.w.) "Msiwaamini Ahlil-Kitab na wala msiwapinge (kuwaambia kuwa ni waongo) semeni tumemuamini Mwenyezi Mungu na yaliyoteremshwa (toka kwake).
Hii inafundisha kutowarejea (Ahlul-kitab) katika mas-ala na (lililopo) ni kuwaacha na kuwapuuza, kwa sababu kutowaamini na kisha kutokuwapinga kunakanusha lengo la kuwauliza ambalo linasubiri jawabu sahihi.
Tatu: Bukhari ameeleza ndani ya Sahih yake katika Kitabut-Tauhidi mlango wa kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Kila siku yeye yumo katika mambo." Juzuu ya nane ukurasa 208 kama ifuatavyo:
Kutoka kwa Ibn Abbas amesema: "Enyi kongamano la Waislamu, vipi mnawauliza Ahlul-Kitab na hali kitabu chenu alichokiteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mtume wenu (s.a.w.) ndicho chenye maelezo halisi ya Mwenyezi Mungu na hakikuharibiwa, Mwenyezi Mungu amekusimulieni kwamba Ahlul-Kitab wamekwisha badilisha na kugeuza (yaliyoteremshwa) katika vitabu vya Mwenyezi Mungu (vilivyotangulia) wakaandika kwa mikono yao kisha wakasema hayo ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili wayauze kwa thamani ndogo, je hajakukatazeni yale yaliyokufikieni katika elimu kuwauliza hao? Basi fahamuni, namuapa Mwenyezi Mungu; hatujamuona mtu miongoni mwao akikuulizeni kuhusu yaliyoteremshwa kwenu."
Nne: Lau leo hii tutawauliza Ahlul-Kitab miongoni mwa Wakristo bila shaka watadai kuwa Isa ni Mungu na Mayahudi wanawapinga (Wakristo kwa madai hayo) na wala hawamkubali (Isa) japo kwa Utume, na kila mmoja wao anaupinga Uislamu na Mtume wa Uislamu, na wanasema kuwa (yeye Mtume) ni muongo na ni mzushi.
Kwa yote hayo basi haiwezekani ifahamike maana iliyomo katika aya kwamba Mwenyezi Mungu ametuamrisha tuwaulize wao, na ilipokuwa Ahlud-Dhikr katika dhahiri ya aya ni wao Ah-Lul-Kitab miongoni mwa Wayahudi na Wakristo, basi hapana shaka hali hii haikanushi kwamba aya hii imeshuka kwa watu wa Nyumba ya Mtume kama ambavyo imethibiti kwa Mashia na Masunni kwa njia sahihi. Kwa hiyo inafahamika kutoka katika aya hiyo kwamba, Mwenyezi Mungu ameirithisha elimu ya Kitabu ambacho ndani yake hakuacha kitu kwa hawa Maimamu ambao amewateua kutoka miongoni mwa waja wake ili watu wawarejee katika Tafsiri na Ta'awiili, na kwa kufanya hivyo uongofu wao utathaminiwa iwapo watamtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na hekima yake imetukuka alitaka watu wote wawanyenyekee wateule wanaotoka miongoni mwao, ambao aliwachagua na akawafunza elimu ya Kitabu ili hali za watu ziwe katika nidhamu. Basi lau watu hawa hawangekuwepo miongoni mwa watu, nafasi ingekuwa wazi mbele ya wenye kujigamba (kuwa wanafahamu), na wajinga na hata kila mmoja angefanya kulingana na matamanio yake na mambo ya watu yangevurugika maadam kila mmoja aweza kudai kuwa ni mjuzi zaidi kuliko mwingine.

No comments:

Post a Comment