Friday 12 September 2014

TOFAUTI ILIYOPO BAINA YA AHLU-SUNNA NA SHIA (ITHNA ASHARI).

Kuna tofauti baina ya Sunni na Shia katika masuala mbali mbali ingawa wote wanaunganishwa na kitu kimoja ambacho ni: Dini Tukufu ya Uislaam. Wote dini yao ni moja yaani Uislaam lakini tofauti ndogo zipo baina yao katika baadhi ya Masuala.
Tofauti kuu iliyopo baina ya Sunni na Shia ni hii ifuatayo:
Ahlu-sunna ambao hujulikana sana sana kwa walio wengi kama (Masunni) hufuata Makhalifa wanne (4) ambao wa kwanza wao ni Abu Abakar bin Kuhafa, na baada ya hao wanne hufuata Makhalifa wote wa Bani Umaiyya (yaani: Makhalifa wale wanaotokana na kizazi cha Bani Umaiyya).
Hivyo Ahlu-sunna wanafuata Makhalifa 4 wa mwanzo, wa kwanza wao akiwa Abu bakari na wa Mwisho wao akiwa Imam Ali (a.s), kisha baada ya hao wanafuata Makhalifa wote wa Banu Umaiyya, hata kama atakuwepo miongoni mwao Khalifa ambaye ni dhalimu, wao wanaamini ni wajibu kufuatwa dhalimu huyo na udhalimu wake sio sababu ya kutofuatwa, kwa ibara nyingine: Uadilifu wa Khalifa sio sharti la kukubalika kwake, bali anaweza kuwa Khalifa na ni wajibu kufuatwa hata kama atakuwa dhalimu na muovu.
Lakini Shia Ithna Ashari, wao ni wafuasi wa Maimam Maasumin Kumi na wawili (12) -a.s- kutoka katika Kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w),hao ndio viongozi wao.
Hivyo Mashia hawaamini Makhalifa zaidi ya kumi na wawili (12) wala idadi pungufu ya kumi na mbili, maana hadithi ya Mtume (s.a.w.w) inasema Makhalifa baada yangu ni kumi na wawili(12), haisemi kuwa makhalifa baada yangu ni wanne (4) au zaidi ya 12.
Hivyo Mashia wanaona kwamba: Kuamini au kufuata Makhalifa wanne Abubakari, omar, Uthamn na Ali, ni kinyume na hadithi ya Mtume (s.a.w.w), maana hadithi hiyo haijasema kuwa Makhalifa ni wanne, bali imesema ni kumi na wawili(12), na akijitokeza mtu akasema: Sunni tunaamini Makhalifa wa kwanza wanne, kisha tunaamini ukhalifa wa makhalifa wa Banu Umaiyya, basi shia Ithna ashari hujibu kunako hilo kuwa kuwa: Makhalifa wa Banu Umaiyya idadi yao ilikuwa zaidi ya 12, wanafika 100 na zaidi, kwa hiyo hiyo nayo itakuwa ni kwenda kinyume na Hadithi ya Mtume (s.a.w.w) kuwa Makhalifa baada yake ni kumi na wawili (12), kwa maana kwamba;Makhalifa hawatakiwi kupungua wala kuongezeka katika idadi hiyo iliyotajwa na Mtume (s.a.w.w) katika hadithi sahihi iliyopokelewa na madhehebu zote za kiislaam.
Hii ndio tofauti kuu inayopatikana baina ya Shia Ithna Ashari na Ahlu-sunna. Kunako tofauti hii unaweza kurejea kitabu kiitwacho:
Tarikh Al-madhahibul-Islamiyya: Juzuu ya 2; ukurasa wa 11-12

3 comments:

  1. Hata nikicomment hamzipablish ...mbona munafanya hivyooo...

    ReplyDelete
  2. Maumbile yetu ni kumuabudu Mola..
    shia suni...ni viumbe tumejitakiya.

    ReplyDelete
  3. Tofauti si juu yetu kuziweka sawa ila ni yy tu Allah.
    ww fundisha lile alilotufunza Muhammad(s.a.w)

    ReplyDelete