Friday 12 September 2014

MIAKA YA MWANZO YA MTUME MOHAMMAD (S.A.W.W)

Ilikuwa ni desturi miongoni mwa Maquraish kuwapeleka watoto wao jangwani kupitisha miaka yao ya mwanzo katika hali ya hewa ambayo ilikuwa ni yenye kutia afya kuliko ile ya Makka. Watoto walijenga miili yenye nguvu zaidi katika maeneo ya wazi na hewa safi ya jangwani kuliko ambavyo wangekuwa katika hewa ya mjini yenye kusonga na kukirihi.
Kulikuwa na sababu nyingine moja zaidi ya kwanini Waarabu wa koo bora waliwapeleka watoto wao kuishi jangwani. Walikuwa wanasisitiza ufasaha katika kuongea na walikuwa "washabiki" wakubwa wa maneno. Walivutiwa na lugha ya Kiarabu, maneno yake, maana zao na tofauti ndogo ndogo katika maana zao; na walijivunia sana katika ufasaha wao binafsi. Kwa kweli, matabaka ya juu katika Makka walipata mamlaka yao juu ya uwezo wao wa balagha. Makka ilikuwa ndio sehemu ya makutano ya misafara mingi na Kiarabu chake kilikuwa kimechafuliwa na kuwa "Kiarabu pijini" (chenye maneno mchanganyiko).
Waarabu wa koo bora hawakutaka watoto wao kujifunza na kuongea kiarabu pijini cha Makka; waliwataka wazungumze tu lugha safi na isiyochanganywa ya jangwani. Wao, kwa hiyo, waliwapeleka watoto wao mbali na Makka ili kuwakinga kutokana na athari zote haribifu kama hizi katika miaka yao ya awali ya maisha yao.
Amina alimtoa mwanae, Muhammad, kwa Halima, mwanamke wa kabila la Banu Asad, aliyekuwa akiishi Mashariki ya Makka, kwa ajili ya malezi. Mtoto mchanga huyu, Muhammad aliishi miaka yake minne ya kwanza ya maisha yake huko jangwani na mama mnyonyeshaji wake. Wakati fulani katika mwaka wake wa tano wa maisha yake, mama huyu anasemekana alimrudisha kwa mama yake huko Makka.
Muhammad alikuwa na umri wa miaka sita wakati Amina, mama yake, alipofariki. Alichukuliwa baadae na Abdul Muttalib, babu yake, mpaka nyumbani kwake. Lakini miaka miwili tu ilipita wakati Abdul Muttalib naye alipofariki.

1 comment:

  1. Asante...tushajuwa hayo
    sasa muhimu....tujuwe ujumbe aliopewa kwetu.

    ReplyDelete