Friday 12 September 2014

Swali la Kwanza kwa Mawahhabi

Kumuona Mwenyezi Mungu na Kumfanyia Mwili
Mwenyezi Mungu katika kitabu chake kitukufu anasema:"Macho hayamfikii (kumuona)". (Qur 'an, 6:103) (Hakuna chochote chenye mfano na yeye) (Qur'an 42:11).
Na anasema Mwenyezi Mungu kumwambia Musa alipotaka kumuona: "Kamwe hutaniona" (Qur'an 7:143.)
Basi ni vipi (enyi Mawahhabi) mnazikubali hadithi zilizopokewa ndani ya Sahih Bukhari na Sahih Muslim kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anajidhihirisha kwa viumbe wake nao watamuona kama wauonavyo Mwezi mpevu?
Na kwamba Mwenyezi Mungu anashuka mpaka kwenye mbingu ya dunia kila usiku na ataweka unyayo wake motoni nao utajaa na kwamba ataonesha mguu wake ili waumini wamtambue na kwamba anacheka na kushangaa, na mengineyo miongoni mwa riwaya ambazo zinamfanya Mwenyezi Mungu kuwa ni mwili wenye harakati na mabadiliko, ukiwa na mikono miwili, miguu miwili na ana vidole vitano, ameziweka mbingu kwenye kidole cha kwanza, ardhi kwenye kidole cha pili, mti kwenye kidole cha tatu, cha nne maji na udongo na kwenye kidole cha tano ameweka viumbe vingine vilivyobakia na anayo nyumba anayoishi ndani yake na Muhammad ataomba ruhusa kuingia humo mara tatu.
Ametukuka Mwenyezi Mungu kwa Utukufu mkubwa kutokana na hayo (hayuko hivyo) utakasifu ni wa Mola wako Mola aliyetukuka kutokana na sifa wanazomzifu.
Jawabu la swala hili liko kwa Maimamu waongofu na Taa ziondoshazo kiza nalo ni kumtakasa kikamilifu Mwenyezi Mungu Mtukufu kutokufanana na umbile na sura na mwili na kumshabihisha na kumuwekea mpaka.
Imam Ali (a.s.) anasema:
"Sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu ambaye wasemaji hawafikii upeo wa sifa zake, wala wenye kuhesabu hawawezi kudhibiti neema zake, wala hawawezi kutekeleza vilivyo haki yake wenye kujitahidi, wala haziwezi kumfikia fikra zozote, na haziwezi kumtambua vilivyo akili mahiri, Mwenyezi Mungu ambaye sifa zake hazina mpaka, wala hasifiki kwa sifa za vilivyopo, na hana wakati unaohesabika wala muda wenye kikomo...
Basi mwenye kumsifu Mwenyezi Mungu Mtukufu atakuwa kamfanyia mwenzi na Mwenye kumfanyia mwenzi, kamfanyia wa pili, na Mwenye kumfanyia wa pili kamgawa mafungu, na amgawaye mafungu basi hamjui Mwenyezi Mungu. Asiyemjua hakika kamuashiria na mwenye kumuashiria kamjaalia mipaka, na mwenye kumjaalia mipaka amemuhesabu, na atakaesema yumo ndani ya kitu fulani, basi kamuambatanisha, na atakayesema yuko juu ya nini kamtoa. Yupo siyo kwa kuzuka, yupo siyo kutokana na kutokuwepo, yu pamoja na kila kitu si kwa wenza naye si kila kitu siyo kwa kumfanya si kitu, mtendaji siyo kwa harakati na vifaa, anaona wakati hakuna kinachomuona miongoni mwa viumbe wake".
Kwa hakika nimeyaelekeza macho ya wachunguzi miongoni mwa vijana wenye taaluma kwenye hazina alizoziacha Imam Ali (a.s.), zilizokusanywa ndani ya Nah-Jul-Balaghah ambacho ni kitabu madhubuti hakitanguliwi ila na Qur'an, na ni kitabu ambacho kwa bahati mbaya hakifahamiki kwa watu wengi kutokana na kampeni, vitisho na vizuizi vilivyowekwa na watawala wa Banu Umayyah na Banu Abbas dhidi ya kila kile ambacho kina uhusiano na Ali ibn Abitalib.
Sitakuwa nimezidisha nitakaposema kwamba ndani ya Nahjul-Balaghah kuna elimu nyingi na mafunzo mengi ambayo watu (wataendelea) kuyahitaji siku zote, na ndani ya Nahjul-Balaghah kuna elimu ya akhlaq, elimu ya jamii, uchumi na miongozo madhubuti katika elimu za dunia na teknolojia na zaidi ya hapo kuna falsafa, tabia, siasa na hekima.
Kwa hakika nimeyathibitisha hayo mimi mwenye we ndani ya Insha niliyotoa kwenye Chuo Kikuu cha Sirbun, Insha ambayo ilijadiliwa juu ya maudhui nne nilizozichagua kutoka ndani ya Nahjul-Balaghah na kutokana na maudhui hizo nilipata shahada ya "Udaktari".
Basi lau Waislamu wangeifuata Nahjul-Balaghah kikamilifu wakayachambua mas-ala yote yaliyomo na kila nadharia, bila shaka (Nahjul-Balaghah) ni bahari yenye kina kirefu, kwani kila aizamiapo mtafiti hutoa ndani yake Lulu na Marjan.
TA'ALIQ (Ufafanuzi): 
Iko tofauti iliyo wazi kati ya Aqida mbili:
Aqida ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa ambayo inamfanya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa na mwili, umbo na sura kama kwamba yeye ni mtu anayetembea na anashuka (kutoka juu) na mwili wake unahifadhiwa na anayo nyumba (anamoishi) na mengineyo miongoni mwa mambo yanayochukiza.
Mwenyezi Mungu ametakasika mno, yu mbali na mambo hayo.
Aqida ya Mashia ambao wanamtakasa Mwenyezi Mungu na kutomfananisha na kumfanyia mwili, na wanasema kuwa haiwezekani kabisa kumuona (Mwenyezi Mungu) hapa duniani wala akhera. Nami binafsi naamini kwamba riwaya wanazotolea hoja Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa zote ni uchafuzi wa Myahudi katika zama za Masahaba, kwani Kaabul-Ahbar Myahudi ambaye alisilimu katika zama za Omar bin Al-Khatab ndiye aliyeingiza itikadi hizi ambazo Wayahudi wanaziamini (na alifanikiwa kwa) kupitia njia za baadhi ya Masahaba wepesi (wa kuhadaika) kama vile Abu-Hurairah na Wahab ibn Munabbah.
Basi ziko riwaya nyingi za aina hiyo zilizopokelewa ndani ya Bukhari na Muslim kutoka kwa Abu-Hurairah, na imekwishatangulia katika uchunguzi uliopita namna gani Abu-Hurairah asivyotenganisha hadithi za Mtume na hadithi za Myahudi Kaabul-Ahbar kiasi kwamba Umar bin Khatab alimpiga na kumzuwia asisiimulie riwaya kuhusu suala la Mwenyezi Mungu kuumba mbingu na ardhi katika siku saba.
Na madam Ahlis-Sunnah Wal-Jamaa wanaziamini Sahih Bukhari na Muslim na kuvifanya kuwa ni vitabu sahihi mno, na maadam hawa wanamtegemea Abu-Hurairah kiasi kwamba amekuwa ndiyo tegemeo la wanachuoni wa hadithi (wa Kisunni) na yeye (Abu-Hurairah) kwa Masunni ndiyo mpokezi wa Uislamu (katika hadithi). Basi kwa hali kama hii haiwezekani kwa Masunni kubadili itikadi yao isipokuwa kama watajikomboa kutokana na kufuata kiupofu, na wakarejea kwa Maimamu waongofu (ambao) ni kizazi cha Mtume nao ndio mlango wa mji wa Elimu ambao huendewa.
Wito huu hauwahusu Wazee na Masheikh, bali kijana mwenye taaluma miongoni mwa Masunni, pia ni miongoni mwa wajibu alionao (kijana) ni kujinasua kutokana na kufuata kiupofu na afuate hoja na dalili.

No comments:

Post a Comment