Friday 12 September 2014

USHUHUDA WANGU JUU YA SHIA WA AHLULBAYT (a.s)

Hapo zamani nilikuwa Muwahhabi kama ninyi nimefunikwa sioni haki wala Ahlul-Bait (a.s.) na wafuasi wao. Mwenyezi Mungu akaniongoza kuelekea kwenye haki ambayo hapana baada yake ila upotovu, na nikawa huru kutokana na minyororo ya ung'ang'anizi na kufuata kama kipofu, na nilifahamu kwamba wengi wa Waislamu bado wamefunikwa na habari zisizo na ukweli na za uzushi. Kampeni zilizoandaliwa kuwapa baadhi ya watu utukufu wasiostahili zinawazuwia (Waislamu) kuufikia ukweli ili wote wapate kupanda meli ya uokovu na washikamane na kamba imara ya Mwenyezi Mungu, na hakuna tofauti kama mjuavyo baina ya Sunni na Shia isipokuwa ni katika yale waliyotofautiana kwa ajili ya Ukhalifa baada ya Mtume, na msingi wa tofauti ni itikadi yao kuhusu Masahaba, nao Masahaba (r.a.) walitofautiana kati yao mpaka wakalaaniana, kupigana na kuuana wao kwa wao. Ikiwa kutofautiana kati yao ni kutoka katika Uislamu basi Masahaba ndiyo wa mwanzo kutuhumiwa kwa tuhuma hii na Mwenyezi Mungu apishe mbali.
Mimi nilistaajabia uadilifu wa wapinzani wa ushia kwani kama ambavyo Mashia wana desturi ya kuwatukuza Ahlul-Bait (a.s.) na kuwaheshimu vile vile Masunni wanayo desturi ya kuwatukuza Masahaba wote, na misimamo hii miwili iko mbali mbali. Kwa nini Shia wakufurishwe kwa kuwaheshimu Mtume na Ahlulbayt wake? Lakini wanaowatukuza Maswahaba wote kwa umoja wao waonekane ndio waislamu sahihi?
Basi ikiwa Mashia kwa desturi yao hiyo wanakosea, basi Masunni ndiyo watakaokuwa wanakosea zaidi (katika desturi yao) kwani Masahaba wote wanawatanguliza Ahlul-Bait (a.s.) kuliko nafsi zao, na huwatakia rehma kama wamtakiavyo rehma Mtume (s.a.w.w.). Na hatumfahamu yeyote miongoni mwa Masahaba (r.a.) aliyeitanguliza nafsi yake au aliyejitukuza juu ya watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) katika elimu au matendo mema.

1 comment:

  1. Asalaam aleykum.
    nakutakia msafara mwema...muhimu tujuwe ALLAH hatizami sura bali Nyoyoni na vitendo vyema.

    ReplyDelete