Friday 12 September 2014

KUTOFAUTIANA KATI YA SHIA NA WAISLAMU WENGINE KULIANZA LINI?

Hitilafu baina ya Shia na Waislamu wengine wasio Shia haikuanza juzi na jana. llianza karne nyingi zilizopita; mara tu baada ya Mtume Muhammad s.a.w.w. kufariki dunia. Hata hivyo, katika kipindi cha Makhalifa wawili wa kwanza, hitilafu hiyo haikuzusha zogo na fitina kubwa kama lile lililozuka katika kipindi cha Makhalifa wa tatu na wa nne.
Baada ya Khalifa wa tatu (Khalifa Uthman) kuuliwa, na mtu aliyekiitwa Muawiya kuongoza upinzani dhidi ya Khalifa wa nne (Imam Ali), ndipo hitilafu hiyo ilipopaliliwa moto. Na kutokana na upinzani huo ndipo Imam Ali a.s. alipolaaniwa, kwa amri ya Muawiya, katika hotuba zote za Ijumaa, kwa muda usiopungua miaka themanini. Ndipo wote wale waliokimtambua Imam Ali a.s. kuwa ni imamu wa haki (yaani Shia) walipokuwa wakisakwa kama nyoka na kuuawa! Ndipo Imam Hassan a.s., mjukuu wa Mtume s.a.w.w., alipouliwa kwa kutiliwa sumu chakulani mwake! Ndipo Imam Hussein a.s., mjukuu mwingine wa Mtume s.a.w.w., alipouliwa kinyama huko Karbalaa (lraq) kwa kukatwa kichwa chake, Kikatungikwa kwenye mkuki na kuchezewa ngoma, na kuliacha pingiti la mwili wake lishetwe-shetwe na farasi! Ndipo hofu ilipofikia kiwango cha watu, chini ya Ufalme wa Muawiya, kuogopa kuwapa watoto walio wazaa jina la Ali! Ndipo hata mashekhe, kwa kuchelea kuadhibiwa na kuuawa, walipokiogopa kulitaja jina la Imam Ali a.s. katika riwaya za Hadith za Mtume s.a.w.w.; badala yake ikawa husema: 'Amesema Sheikh'!

No comments:

Post a Comment